Habari za Punde

Walimu waagizwa kutumia zana sahihi za kufundishia

 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi Asya Iddi Issa akizungumza wakati wa kuyazindua maonesho ya Tatu ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia yaliyoandaliwa na wakufunzi wa Chuo cha Kiislamu (CCK) Mazizini mjini Unguja.
Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Kiislamu Bakari Choum akizungumza macxhache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi Asya Iddi Issa kuyazindua maonesho ya Tatu ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia yaliyoandaliwa na wakufunzi wa Chuo cha Kiislamu (CCK) Mazizini mjini Unguja.
Wanafunzi wa Chuo cha Kiislamu wakiwa katika uzinduzi wa maonesho ya Tatu ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia yaliyoandaliwa na wakufunzi wa Chuo cha Kiislamu (CCK) Mazizini mjini Unguja.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhururia uzinduzi wa maonesho ya Tatu ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia yaliyoandaliwa na wakufunzi wa Chuo cha Kiislamu (CCK) Mazizini mjini Unguja.


 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi Asya Iddi Issa amesema uhalisia wa matumizi sahihi wa zana za kufundishia ni njia moja wapo ya kuwafanya Wanafunzi kuelewa kwa vitendo wanachofundishwa darasani.

Akizungumza wakati wa maonesho ya Tatu ya vifaa vya kufundishia na kujifuzia yaliyoandaliwa na wakufunzi wa Chuo cha Kiislamu (CCK) Mazizini mjini Unguja.
Amesema hakuna mada isiyohitaji zana za kufundishia, hivyo ni lazima walimu wanapoingia darasani kuingia na zana zao za kufundishia na si lazima ziwe zana za kununua lakini ni vyema watumie ubunifu wao ili waweze kufikisha vizuri elimu kwa wanafunzi wao.
Hata hivyo Bi Asya ameahidi kushirikiana na Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu katika kuhamasisha umuhimu wa kutumia zana za kufundishia madarasani na kuhakikisha zana hizo zinafanyiwa kazi kiusahihi.
Aidha amewapongeza walimu wa Chuo hicho pamoja na wakufunzi kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuandaaa maonesho hayo na kuwataka kuendelea kuyafanyia kazi katika Skuli watakazokwenda kusomesha ili kuweza kuzalisha watoto bora watakaokuwa viongozi wazuri wa baadae katika Taifa hili.
Nae Mkurugenzi Idara ya Mafunzo ya Ualimu Bi Maimuna Fadhil Abasi amesema amefarajika kuona walimu wamejitoa kuwafundisha Wanafunzi kwa vitendo na kuwataka walimu kutengeneza zana sahihi kwa wanafunzi ili kuwapa uelewa wa haraka Wanafunzi wao.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho ndugu Bakari Choum Ame, amesema wamejitahidi kubuni na kutengeneza vifaa mbali mbali vya kufundishia ili wakufunzi hao wanapofika sehemuu zao za kazi waweze kufundisha vizuri zaidi na kwa umakini.
Mapema akisoma risala kwa niaba ya wakufunzi wenziwe Mkufunzi Nasir Ali Ziadi amesema mafunzo hayo yameweza kuwajengea ubunifu na uwezo katika kufundishia, hivyo wameuomba uongozi wa Chuo kuengeza bajet katika kuboresha maonyesho ya vifaa vya kujifunza na kufundishia kwa ili yaweze kukua zaidi.
Maonyesho hayo ya tatu ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia yamebeba kauli mbiu "Mwalimu tengeneza zana sahihi kujenga dhana kwa wanafunzi" ambapo yameenda sambamba na na zoezi la upimaji afya bure kwa maradhi ya kusukari, shindikizo la damu, upimaji wa uzito na urefu pamoja na uchangiaji wa damu wa hiari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.