Habari za Punde

Madiwani wa Mkoa wa Kusini na Wanafunzi wa Skuli ya Glorious Academy Watembelea Ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani kwa Ziara ya Kujifunza.

Mwakilishi wa Jimbo la Shaurimoyo Mhe Hamza Hassan Juma akiwafahamisha Wanafunzi wa skuli ya Glorious Academy dhana ya Uchumi wa Buluu wakati walipofika katika Ofisi ya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya ziara ya kimasomo kuhusu shughuli za Baraza la  Wawakilishi Zanzibar .
Kaimu Mkuu wa Idara ya Shughuli za Baraza na Ushauri wa kisheria Baraza la Wawakilishi Ndg.Othman Ali Haji akiwasilisha mada  kuhusu mbinu za kujenga na kuibua hoja katika utekelezaji wa kazi za Madiwani wakati alipokutana na Madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya Kusini Unguja walipotembelea katika ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani ikiwa ni sehemu ya kujijengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.