Habari za Punde

Makamu wa kwanza wa Rais, Mhe Othman Masoud amtembelea Mzee Machano Khamis

Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Othman Masoud Othman Sharif amemtembelea Mzee Machano Khamis nyumbani kwake Mombasa Zanzibar leo kumjuulia hali.
Mzee Machano Khamis alikuwa ni miongoni mwa wanasiasa waliokuwa wakimuunga mkono Maalim Seif Sharif ( Allaah Amrehemu) alipokuwa Kamishna wa Polisi na Maalim ni Waziri Kiongozi.

Mzee Machano ambae sasa ni mgonjwa aliwahi kushika wadhifa wa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa chama cha CUF.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.