Habari za Punde

Sherehe za kuapishwa kwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman Ikulu leo 2-3-2021.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mteule Mhe. Othman Masoud Othman akiwasili Ikulu kwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi  katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. 
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mteule Mhe. Othman Masoud Othman akiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar akisubiri kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika leo 2-3-2021.Ikulu Zanzibar 
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe.Zuberi Ali Maulid na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji, wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masod Othman, iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mteule Mhe.Othman Masoud Othman, iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 2-3-2021.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mteule Mhe. Othman Masoud Othman akiwa amesimama wakati ukipigwa Wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla ya kuapishwa iliofanyika leo 2-3-2021, katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Othman Masoud Othman kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. leo 2-3-2021.
WAKUU wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar na Viongozi wa Dini wakifuatilia kuapishwa kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Mhe. Othman Masoud Othman, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akisaini hati ya kiapo baada ya kumalizika kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Hussein Ali Mwinyi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha na pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar waliosimama nyuma na waliokaa kutoka (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha na pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa waliosimama nyuma na waliokaa kutoka (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman,baada ya kumalizika kwa hafla ya kuapisha iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia kwa Rais) na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla.baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, baada ya kumalizika kwa kuapisha katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.