Habari za Punde

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango akutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Indonesia nchini. Neema ya kuwekeza yanukia


 Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi

Zanzibar
, Mheshimiwa Jamal Kassim Ali amefanya mazungumzo na Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Prof. Ratian Pardede.
Katika mazungumzo hayo Mhe.
Jamal Kassim
amesema Serikali ya Awamu ya nane imetangaza Sera ya Uchumi wa Blue na ameyataja maeneo muhimu ya Uwekezaji Nchini kuwa ni Ujenzi wa Bandari Mpya ya kisasa ya Mangapwani, Bandari ya Mpigaduri, kuimarisha sekta ya Utalii, Uvuvi, Viwanda kwa upande wa Unguja, upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa
Pemba
Pamoja na kuimarisha sekta ya Utalii wa Mazingizra (E-co Tourism) sambamba na uwekezaji katika eneo la Mkumbuu kwa Upande wa
Pemba
.
Aidha, Mheshimiwa Jamal ameitaka Indonesia kuja kuwekeza
Zanzibar
katika Sekta mbali mbali, zikiwemo sekta ya Mafuta na Gesi, Utalii wa Mazingira kisiwani Pemba.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Afisi ya Rais Fedha na Mipango
Zanzibar
.
Nae Muheshimiwa Balozi wa Indonesia Prof. Ratian Pardede, amesema Nchi yake imekusudia kuja kuekeza Zanzibar na imetenga jumla ya fedha za Kimarekani Dola Milioni arubaini (USD 40) kwa ajili ya kuwekeza Zanzibar katika sekta ya viwanda.
Balozi Ratian, alieleza kuwa Serikali ya Indonesia tayari imeshatenga fedha nyengne Jumla ya Dola za Kimarekani Milioni mia moja na tisiini (USD 190) kwa uwekezaji
Zanzibar
katika sekta mbali mbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.