Mwashungi Tahir Maelezo 15/3/2021.
Wanawake nchini wametakiwa kuwa na tabia ya kupima afya zao na kushiriki kufanya mazoezi ili kujilinda na maradhi yasiyo ambukiza.
Akizungumza na wanachama wa chama hicho Daktari wa maradhi bingwa yasioambukiza Salama Asaa Ali kutoka Mnazi Mmoja katika Ukumbi wa Tamwa ulioko Tunguu wakati wa mkutano mkuu wa waandishi wa habari wanawake na kutoa elimu ya afya kwa lengo la kujitambua mapema afya zao na kupatiwa matibabu haraka.
Amesema baadhi ya akinamama wengi hawana tabia ya kufika vituoni kupima afya zao kwani inasaidia unapogundilika unaanza kuwa na maradhi yataweza kutibika kwa haraka kabla hayajakithiri ndani ya miili yao.
Hivyo amesema hivi sasa kuna maradhi mengi duniani ikiwemo kisukari, kensa, presha na kuwaomba kula vyakula vya matunda , kunywa maji kwa wingi na kuepuka kula vyakula vya mafuta mara kwa mara ili kuepukana na maradhi hayo.
Nae Mkurugenzi wa waandishi wanawake Tamwa, Dr Mzuri Issa amesema ametaka wanawake kupatiwa elimu hiyo kwa lengo la kupima ili kujitambua mapema na kufanyiwa matibabu.
Nao wanachama wa mkutano huo wa Tamwa wameishukuru jumuiya hiyo kwa kuwapatia elimu hiyo ambayo itawafanya kuhamasika kupima afya zao pale mtu akiona zile dalili zilizotajwa anazo ili kupatiwa matibabu.
Aidha elimu nyengine iliyotolewa hapo ni pamoja na changamoto za uzazi,shingo ya kizazi, tezi dume, matatizo yanayosababisha kukosekana kwa hedhi, figo na mengi mengineo.
Mkutano huo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kujadili mikakati na maendeleo ya chama hicho cha waandishi wa habari wanawake Tamwa ambao ulifanyika siku mbili huko Tunguu Zanzibar.
No comments:
Post a Comment