Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Machi 19, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdalla (wa tatu kushoto) wakimsiliza Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) , Meja Jenerali, Charles Mbuge (kulia) ambaye alikuwa akitoa maelezo kuhusu maandalizi ya maombolezo ya kifo cha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, Machi 19, 2021. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, na watano kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Bashiru Ally.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment