Habari za Punde

KATIBU MKUU NZUNDA AHIMIZA KASI NA MATOKEO OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Profesa Jamal Katundu akizungumza na Menejimenti ya Ofisi hiyo upande wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu mara baada ya kuwasili katika ofisi hiyo  Aprili 8, 2021 eneo la Mtumba Jijini Dodoma.(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na: Mwandishi Wetu – Dodoma

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) amewataka Manaibu Makatibu Wakuu wapya, Menejimenti  na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza kasi, bidii na ari katika utendaji kazi wa majukumu ili kutoa matokeo yenye tija  kwa wananchi.

Katibu Mkuu Nzunda ameyasema hayo leo tarehe 8 Aprili, 2021, Jijini Dodoma, wakati wa kuwapokea Manaibu Makatibu Wakuu wapya wa Ofisi ya Waziri Mkuu walioapishwa Ikulu Jijini Dar Es Salaam, Aprili 6, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Ameeleza kuwa, Ofisi hiyo ina majukumu makubwa ikiwemo kuratibu shughuli za Serikali, hivyo ni muhimu kuongeza nguvu zaidi katika utekelezaji wa majukumu ili kusimamia kwa ufanisi uratibu wa shughuli za serikali.

“Jukumu letu ni kumsaidia Mhe. Waziri Mkuu kutekeleza majukumu ya kusimamia shughuli za serikali, hatunabudi kufanya kazi kwa utaalamu, weledi na kwa kuwajibika kwa kujituma ili kuhakikisha matokea anayo yataka,” alisema Nzunda

Kwa upande wa Manaibu Makatibu Wakuu wapya; Profesa Jamal Adam Katundu na Kaspar Kaspar Mmuya. wameahidi  kushirikiana na Watendaji wa Ofisi hiyo kumhakikishia  Katibu Mkuu huyo kuwa wapo tayari kufanya kazi kwa  kasi ili kupata matokeo chanya kama ilivyo kusudiwa.

Tarehe 6 Aprili, 2021 Ikulu Jijini Dar Es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwaaapisha Manaibu Makatibu Wakuu wa Ofisi hiyo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.