Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe.Simai Mohammed Said Akabidhi Vifaa vya Ujenzi Jimboni.

Mwakilishi wa Mwakilishi wa jimbo la Tunguu ambae pia ni Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said  (katikati) akikabidhi mipira ya kusambazia maji safi na salama kwaadhi ya wananchi wa jimbo hilo, ikiwa ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa kwa wananchi wake katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita.

Mwakilishi wa  jimbo la Tunguu kupitia Chama cha Mapinduzi ambae pia ni Waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said amekabidhi  vifaa mbali mbali vya ujenzi kwa wananchi wa jimbo hilo vyenye thamani ya shilingi milioni 16.

Akikabidhi vifaa hivyo katika tawi la CCM Tunguu, mhe Simai amesema ameamua kuendelea kutekeleza ahadi alizozitoa kwa wananchi wake wakati katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita.

Amesema ana imani kuwa vifaa alivyovitoa vitaweza kusaidia katika kupunguza changamoto mbalimbali katika jimbo hilo zikiwemo tatizo la upatikanaji WA huduma ya maji safi na salama katika baadhi ya shehia za jimbo hilo.

Aidha Mhe Simai amewaomba wananchi hao kuendelea kudumisha Amani na utulivu WA nchi pamoja na kukichagua chama cha Mapinduzi katika chaguzi zake katika ngazi zote.

Hata hivyo Mhe Simai amewaahidi wananchi wake kuendelea kuwatumikia bila ya kujali itikadi zao za vyama au dini, kusema kuwa yeye ni kiongozi wa wananchi wote.

Nao baadhi ya wananchi wa jimbo hilo wamempongeza Mhe Simai kwa uamuzi aliouchukua WA kuendelea kutekeleza ahadi zake na wamemuahidi kumuunga mkono pamoja na kukipigania chama cha Mapinduzi ili kibaki madarakani.

Mhe simai amekabidhi mipira ya kusambazia maji safi na salama, gari kwa ajili ya kusaidia wagonjwa na shughuli za kijamii, mabati kwa ajili ya  kuezekea Tawi la CCM, pamoja na fedha taslim kwa vikundi mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza kilimo pamoja na ujasiriamali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.