Habari za Punde

ZFDA Yateketeza Tani 42.5 za Mchele Ulioharibika Ulioingizwa Zanzibar.

Baadhi ya mafiasa kutoka Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) wakishuhudia mchele aina Chereko mapembe ulioharibika ukishushwa toka kwenye magarini tayari kwa uteketezwaji katika Jaa la Kipele liliyopo Mkoa wa Kusini Unguja.
Gari aina ya Kijiko likifukia shehena za mchele uharibika ambao haufai kwa matumizi ya binadamu katka Jaa la Kipele.

Mkuu wa Usajili na Tathmini ya Chakula kutoka ZFDA Khadija Ali akifanya mahojiano na wandishi wa habari juu ya kukamatwa kwa mchele huo.

Picha na Makame Mshenga.

Na Ramadhani Ali – Maelezo. Zanzibar  20.04.2021

Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) imeteketeza tani 42.5 za Mchele wa mapembe aina ya Chereko ulioingizwa nchini kutoka India na Kampuni ya Zenj General Mechandiser baada ya kubainika umeharibika na haufai kwa matumizi ya binadamu.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuuteketeza katika Jaa la Kibele, Mkoa wa Kusini Unguja, Mkuu wa Usajili na Tathmini ya Chakula wa ZFDA Khadija Ali alisema mchele huo ulikuwa unaendelea kuuzwa na walipata taarifa kutoka kwa wananchi walionunua.


Alisema walifanya ukaguzi na kugundua kkuwa Kampuni ya Zenj General Mechandiser liliopo Fuoni meli tano ndio inayomiliki mchele huo na ulikuwa ukihifadhiwa katika ghala lake liliopo Fuoni meli tano.


Mkuu wa Usajili na Tathmini ya Chakula Khadija Ali alisema Taasisi hiyo itaendelea kufanya ukaguzi wa bidhaa zinapokuwa bandarini na kufanya ufuatiliaji madukani na katika maghala ili kuhakikisha bidhaa zilizoharibika na kumaliza muda wa matumizi haziingii sokoni.


Alieleza kuwa moja ya jukumu la Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi ni kuona wananchi wanauziwa bidhaa zilizo salama kwani wanapotumia bidhaa zilizoharibika wanaweza kupata matatizo ya tumbo na hata maradhi ya Kensa


Aliwashauri wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa, hasa kwa njia ya mtandao, kuwa waangalifu na kuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi bidhaa zinapofika nchini kwani zinaweza kuharibika ikiwa utaratibu wa kuhifadhi katika maghala hautafuatwa.


Mfanyakazi mmoja wa Kampuni ya Zenj General Mechandiser aliekuepo wakati wa kuangamiza mchele huo alishindwa kueleza chochote licha ya kutakiwa atowe maelezo kuhusu kuharibika mchele huo.


Afisa Mazingira kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar Muhsini Ali alisema Ofisi hiyo inalazimika kusimamia zoezi la kuharibu chakula kibovu ili kuhakikisha linakamilika na linafanywa bila ya kuathiri mazingira ya eneo husika.


Alisema kipindi kilichopita waliwahi kutokea wananchi kuchukua mabaki ya bidhaa zilizoharibiwa na kwenda kuzitumia jambo ambalo linaweza kuathiri afya zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.