Habari za Punde

*MWENEZI SHAKA AUNGANA NA WAISLAMU KATIKA SWALA YA EID AL- FITRI , UJIJI - KIGOMA*

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka ameshiriki swala ya Eid Al-Fitr na waumini wa Dini ya Kiislam Mkoa wa Kigoma iliyosaliwa katika Uwanja wa Stendi Mpya ya Ujiji-Kigoma mapema leo tarehe 14 Mei 2021.




Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka ameshiriki swala ya Eid Al-Fitr na waumini wa Dini ya Kiislam Mkoa wa Kigoma iliyosaliwa katika Uwanja wa Stendi Mpya ya Ujiji-Kigoma mapema leo tarehe 14 Mei 2021.

Swala hiyo iliyoongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Sheikh Hassan Kiburwa ilihudhuriwa pia na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wa zalendo Ndugu Juma Duni Hajji, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Ndugu Suleiman Jafo, Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini Ndugu Kilumbe Shaban Ng'enda,  Mbunge wa Sumbawanga mjini Ndugu Aeshi Hillary na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Ndugu Maryam Ditopile. 

Katika salamu zake za Eid Al-Fitr kwa waumini wakati wa Swala, Mwenezi Shaka amefikisha salamu za Eid kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan, ambapo amewaambia waumini kuwa;

"Mwenyekiti wetu na Rais wenu mpendwa amenituma niwaeleze kuwa anawapenda na anawatakia heri na furaha katika siku muhimu  duniani"

Mwenezi Shaka amewaomba waumini kuliombea Taifa pamoja na kumuomba MwenyeziMungu amjaalie Mwenyekiti wa CCM na Rais wetu Ndugu Samia Suluhu Hassan, ampe Afya njema, maono na msimamo thabiti katika kuiongoza nchi yetu.

Aidha, Mwenezi amewataka  wananchi kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii ili tuweze kuzalisha ili kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa Taifa, sambamba na kutimiza kutunza na kuimarisha hali ya amani, utulivu, umoja na Mshikamano katika nchi yetu.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.