Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo
akitoa maelekezo Mkurugenzi wa Kiwanda cha Lodhia Steel Industry Ltd. Bw. Sailesh Pandit mara baada ya kufanya
ziara ya kikazi Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha Lodhia Steel Industry Ltd.
Bw. Sailesh Pandit akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo kuhusu shughuli za uendeshaji
na hifadhi ya mazingira kiwandani hapo, Waziri Jafo hii leo amefanya ziara ya
kikazi katika Wilaya ya Mkuranga kujionea uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwasili
katika Kiwanda cha Nondo cha Lodhia kilichopo katika Wilaya ya Mkuranga, Mkoa
wa Pwani. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkurunga Bw. Filberto Sanga na Bw. Sailesh
Pandit Mkurugenzi wa Kiwanda hicho.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akitoa
maelekezo kwa Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) Kanda ya Mashariki kusini Bw. Hamad Taimur (hayupo pichani) kuhusu
Kiwanda cha Saruji cha Diamond ambacho kimekithiri kwa uchafuzi wa mazingira.
Waziri Jafo amefanya ziara hiyo leo Mei 4, 2021. Watatu kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Mkurunga Bw. Filberto Sanga.
No comments:
Post a Comment