Habari za Punde

Idadi ya wageni wa utalii yaongezeka

Na  Mwashungi Tahir,         Maelezo    

Jumla ya wageni 9,280 waliingia nchini kwa mwezi wa Mei, 2021 ukilinganisha  na wageni 197 walioingia nchini  kwa mwezi  Mei,2020  ambapo ukilinganisha nawageni 13,839 walioingia nchini katika mwezi wa April,2021 ikiwa ni upungufu wa asilimia 32,9.


Akiwasilisha Takwimu za uingizaji wa wageni kwa mwezi wa Mei,2021 Mkuu wa Idara ya za Takwimu za Kiuchumi Abdul Ramadhani Abeid kutoka Afisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar amesema hali inaonyesha upungufu wa asilimia 32.9 ukilinganisha na wageni 13.839 walioingia nchini kwa mwezi wa April 2021.


Amesema Nchi inayoongoza kuleta watalii ni Afrika Kusini  ambapo jumla ya wageni 782 sawa na asilimia 8.4 kwa wageni  ambapo ni kwa mara ya kwanza kuleta kiwango hicho soko ambalo linaanza kukua kwa kuleta watalii ikifuatiwa na Ufaransa walikuwa watalii 680 sawa na asilimia 7.3.


Amesema  kwa upande wa wageni kwa bara na nchi nyengine walizotoka jumla ya wageni 4,508 walioingia nchini kutoka Bara la ulaya sawa na asilimia 48.6 ya wageni wote wa mwezi Mei, 2021


Aidha amesema kwa mwezi Mei, 2021 jumla ya wageni 6,874 sawa na asilimia 74,1 ya wageni waliingia Zanzibar kupitia viwanja vya ndege  na wageni 2,406 sawa na asilimia 25.9 waliingia kupitia Bandarini ambapo wanaume 4,960 sawa na asilimia 53.4 na wanawake 4,320 sawa na asilimia 46.6 ya wageni waloingia nchini.


Nae Mhadhir wa Uchumi SUZA,  Dr Stela Ngoma Hassan  amesema wageni wengi kutoka Afrika ya Kusini wanakuja huku kutokana na nchi yao kuwa na baridi kali  sana.


Vile vile Mrakibu Msaidizi Uhamiaji Rashid Abdullah Ali amesema Idara ya Uhamiaji imezidi kuboresha huduma kwa wageni kwa kusimamia usalama wao pamoja na afya zao na kuhakikisha wanakuwa salama.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.