Habari za Punde

Makamu wa Rais Dk Mpango akamilisha ziara yake kisiwani Pemba

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akitembelea  ujenzi wa Nyumba za Makazi za Polisi  zinazojengwa katika kijiji cha Mfikiwa Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba, wakati Makamu wa Rais Dkt. Mpango alipokuwa katika mfululizo wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili iliyomalizika leo Juni 15,2021.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mohammed Haji Hassan akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Nyumba za Makazi za Polisi  zinazojengwa katika kijiji cha Mfikiwa Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba, wakati Mmakamu wa Rais Dkt. Mpango alipokuwa katika mfululizo wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili iliyomalizika leo Juni 15,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akizungumza na Askari wa Jeshi laPolisi  na Wananchi wa Kijiji cha Mfikiwa Kisiwani Pemba baada ya kutembelea ujenzi wa Nyumba za Makazi za Polisi  zinazojengwa katika kijiji hicho Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba leo Juni 15,2021.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akikabidhi Fedha Taslim  kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba ACP Jums Said Khamis kwa ajili ya ukamilishaji wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Polisi  zinazoendelea kujengwa katika kijiji cha Finya  Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo Juni 15,2021.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akiweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi zinazojengwa katika Kijiji cha Finya   Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba leo Juni 15,2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akijumuika kucheza ngoma ya Msewe na Wananchi wa Kijiji cha Finya Kisiwani Pemba wakati alipofika katika Kijiji hicho kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Polisi leo Juni 15,2021
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akiagana na Viongozi mbalimbali wa Serikali Kisiwani Pemba kwenye Uwanja wa ndege wa ChakeChake Pemba baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi ya siku 2kisiwani humo leo Juni 15,2021.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.