Habari za Punde

Naibu Waziri Mhe.Kipinga Atembelea Waliomaliza Chuo Kikuu Vinara na Ufugaji Kuku Dodoma.

Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma unavyoonekana wakati wa maonesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vilivyo chini ya NACTE na taaisisi nyingne.

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa (kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga alipotembelea banda la NIT kwenye maonesho ya vyuo vya elimu ya mafunzo na ufundi kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa kituo cha umahiri katika usafiri wa anga na operesheni za usafirishaji, Mhandisi Abubakar Noor.

Mkurugenzi wa uthibiti, ufuatiliaji na tathimini wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Dkt. Jofrey Oleke  akizungumza na wawakilishi wa taasisi zilizoshiriki manonesho ya pili ya mafunzo na ufundi yanayofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma, ili kupata maoni yao katika kuboresha maonesho yatakayofuata. Maonesho hayo yameandaliwa na NACTE.

Mwenyekiti wa Baraza la NACTE Prof. John Kondoro (kulia) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga alipotembelea maonesho ya elimu ya mafunzo na ufundi kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, yaliyoandaliwa na NACTE. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa NACTE, Dkt. Adolph Rutayuga.

 

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM

 0754264203

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.