RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mgeni wake Balozo wa Uturiki Nchini Tanzania Mhe. Mehmet Gulluoglu, akimshindikiza baaba ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alikutana na kufanya mazungumzo na
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dk. Mehmet Gulluoglu.
Dk. Mwinyi alisema kutokana na mashirikiano yaliopo kati ya nchi mbili hizo, ana imani kubwa kuwa Wawekezaji kutoka Uturuki watashajihika na kuja nchini kwa ajili ya kuwekeza katika nyanja tofauti, pale hali ya ugonjwa ya Covid -19 itakapopungua.
Nae, Balozi Mehmet aliahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano ulipo kati ya nchi mbili hizo, sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha sekta za Uwekezaji , Utalii, Uvuvi pamoja na Mafuta na Gesi.
Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822
E-mail:
abdya062@gmail.com
No comments:
Post a Comment