Habari za Punde

Uzinduzi wa Website ya Mfuko wa Uwezeshaji Kiuchumi Zanzibar.

Na Ali Issa - Maelezo Zanzibar 12/6/2021.

Mkurugenzi wa Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanznzibar Ndg.Suleiman Ali Haji amesema njia rahisi ya kuwawezesha wananchi kuinuka kiuchumi na kuimarisha hali zao kimaisha ni kujiunga na vikundi vya ushirika vinavyoazishwa majimboni.


Hayo ameyasema leo huko Kariakoo Mjini Unguja wakati wa Uzinduzi wa website ya Uwezeshaji SACCOS LTD katika mkutano Mkuu wa mwaka.


Amesema hali hiyo itawasaidia sana wananchi kupata mikopo ya uhakika ili kujikwanua na umasikini na kuondokana na utegemezi


Amewasisitiza wananchi  kujiunga na vikundi hivyo kwani husaidia kutoa mikopo na kuwapa mitaji ya kufanya biashara  ili kujiendeleza na kupata maendeleo mazuri katika maisha yao.


Mkurugenzi Suleiman ameeleza kuwa  nchi za ulimwengu wa watatu zinasonga mbele kwa kufuata mfumo wa kuwajengeea uwezo wananchi kwa kuazisha vikundi vya ushirika ili kusaidia kuondokana na utegemezi kwa jamii.


‘’Vikundi vya ushirika hubarikiwa sana na hata na benki kwa vile wamejikusanya kwa wingi na kuzalisha mitaji mikubwa ambayo huaminika kwa kupewa mikopo ya kujikimu ili kujinasua umasikini”, alifahamisha Mkurugenzi hyo.


Nae msoma Risala ya SACCOS hiyo akitaja mafanikio walioyapata wananchi wao nipamoja na kuwezesha kutoa mikopo 774 yenye thamani ya shilingi Bilioni tatu milioni mia sita kuminasita lakimoja sitini elfu.


Hata hivyo alisema SACCOS yao inamtaji wazaidi ya Bilioni moja ulio patikana kwa nguvu za wanachama 586, wanawake 246 na 247 wanaume.


Akitaja changamoto zinazo wakabili ni pamoja na kutakiwa kulipa kodi kwa taasisi mbalimbali kama vile tume ya ushindani halali,TRA,ZRB,BPRA, na kadhalika.


Badria alisema kadhia hiyo inawapa shida sana hasa wakizingatia wanachama wao ni wanyonge ambao wamekimbilia utaratibu wa kukopeshana wenyewe kwa wenyewe ili kutafuta unafuu wa maisha yao.


Uwezeshaji  SACCOS LTD imeazishwa kwa muungano wa SACCOS mbili UWAVISACOS na USHIKAZISACCOS baada ya kuundwa Wizara ya kazi uwezeshaji wananchi kiuchumi na ushirika mwaka 2010, baada viongozi kugundua kuna SACCOS mbili katika Wizara moja na 2011 kuziunganisha kua moja, iliazia na  wanachama 120 na kua thamani ya shilingi milioni 30.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.