Habari za Punde

Wafanyakazi watano wa ZAWA mikononi mwa Polisi kwa tuhuma za wizi wa mabomba

Na Mwandishi wetu 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja linawashikili watuhumiwa Saba (7) kwa wizi wa Mali ya Serikali kati yao Watano ni wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Zawa akiwemo Mkurugenzi wa Ufundi na Miundombinu wa Mamlaka hiyo 

Akitoa taarifa kwa Vyombo vya habari kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Awadh Juma Haji huko ofisini kwake MwembeMadema Mjini Unguja

Kamanda Awadha amesema mnamo tarehe 27 Mei 2021 majira ya saa 2:00 Asubuhi huko katika ofisi za Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA iliyopo maeneo ya Saateni waligundua kuibiwa kwa mabomba ya Maji 46 yenye ukubwa tofauti yanayokadiriwa kuwa na thamani ya TSH Milioni thelathini (30,000,000) na mota 30 za kusukuma maji zinazokadiriwa kuwa na thamani ya TZSH Milioni Hamsini (50,000,000)  Mali ya ZAWA

"Tukio hilo limeripotiwa Poliei Tarehe 30 Mei 2021 na mara baada ya tukio hilo kuripotiwa msako mkali ulifanyika na kufanikiwa kukamata mabomba yote 46 na watuhumiwa wawili wanaojihusisha na biashara ya uuzaji wa Vyuma chakavu katika maeneo ya Garagara Wilaya ya Magharib A, upelelezi uliendelea na kufanikiwa kukamata watuhumiwa wengine watano ambao ni wafanyakazi wa ZAWA" alisema kamanda  Awadh


Akiwataja watuhumiwa hao kamanda Awadh amesema ni pamoja na Bakari Shaabani Shauri ambae ni mfanyabiashara wa vyuma chakavu,Alawi Nassir Alawi ambae ni Mfanyabiashara 


Wengine waliokamatwa kwa tuhumza hizo ni wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ambao ni Mhandisi Hassan Khamis Hassan,Bakari Mohammed Bakari,Ally Chande Ally,Seth Idrisa Nahoda na Khalfan Omar Juma ambapo alisema bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukip hilo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.