Habari za Punde

Wakulima Wadogo Kunufaika na Mikopo ya Kilimo Kupitia Benki ya NBC.

 

Meneja wa Maendeleo ya Biashara ya Benki ya  NBC Tanga Aljiran Mbwani akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maonyesho ya biashara ya Tanga
Meneja wa Maendeleo ya Biashara ya Benki ya  NBC Tanga Aljiran Mbwani wakati wa maonyesho ya biashara ya Tanga akipokea cheti kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Hassani Mnyima
Meneja wa Maendeleo ya Biashara ya Benki ya  NBC Tanga Aljiran Mbwani wakati wa maonyesho ya biashara ya Tanga kulia akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga aliyetembelea banda lao

WAKULIMA wadogo wadogo waliopo kwenye vikundi vya Ushirika (Amcos) wanatarajiwa kunufaika na mikopo ya Kilimo inayotolewa na Benki ya ya Taifa ya Biashara (NBC) ili kuweza kuwa na akauti za benki na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Maendeleo ya Biashara ya Benki ya  NBC Tanga Aljiran Mbwani wakati wa maonyesho ya biashara ya Tanga ambapo alisema wameingia mkataba na benki ya wakulima (TADB)  na wametenga kiasi cha Bilioni 200.

Alisema fedha hizo ni kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo na wanaowaangalia wale waliopo kwenye vukundi vya vyama vya ushirika (AMCOS)wanawasaidia kwa sababu taarifa zao zinakuwa

Meneja huyo alisema walichopeleka  kwenye maonyesho hayo ni akauti kwa ajili ya wakulima kama dhima ya mwaka huu  ya kilimo ndio msingi wa viwanda inavyosema kuwawezesha wakulima waweze kuwa na akauti za benki   walau waweze kutimiza vigezo moja wapo wakati wakihitaji kupata mikopo.

Alisema kwa hiyo mkulima atakapokuwa na akauti hizo ambazo zinaghamara nafuu atakuwa na uwezo wa kufanya miamala ya kibenki lakipi pia kuweza kupata fursa ya kupata mikopo midogo na mikubwa .

“Kwanza tulianza na wakulima wakubwa tulikuwa wanawapatia matrekta lakini pia tumeingia mkataba na benki ya TADB  na tumetenga kiasi cha Bilioni 200 kwa ajili ya wakulima wadogo wadogo kupitia Amcos hivyo nitoe wito kwa wakulima wakubali kufungua akauti benki na manufaa yake ni makubwa na yajayo yanafurahisha kupitia shughuli zapo za kilimo watanufaika na huduma nzuri za benki na mikopo mwisho wake kuweza kukuza kipato kwenye biashara zao”Alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.