Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akikagua na kutoa
maelezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa kufua umeme wa Mwalimu Julius
Nyerere juu ya uzingatia wa Kanuni za Mazingira za Udhibiti wa Taka hatarishi
na Taka za Kielekroniki za mwaka 2021. Waziri Jafo ameelekeza taka hizo ikiwa
ni pamoja na chuma chakavu kuuzwa wa wafanyabiashara wenye vibali tu
Mhandisi Mkazi kutoka
Taasisi ya TEKU - TANROADS John Mageni akitoa maelezo ya kitaalamu kwa Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo mara
baada ya kufanya ziara ya kikazi kwa lengo la kukagua uzingatiaji wa masharti
yaliyowekwa katika Cheti cha Tathmini ya Mazingira katika ujenzi wa Mradi wa
kufua umeme wa Mwalimu Julius Nyerere. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la
Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Dkt. Samwel Gwamaka.
Picha zikionyesha hatua mbalimbali za ujenzi wa Mradi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere. Ujenzi huo umefikia asilimia 54 ya utekelezaji kati ya asilimia 59 zilizokusudiwa na unaratajiwa kukamilika
|
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Selemani Jafo ameridhishwa na uzingatiaji wa Sheria ya mazingira katika
kutekeleza Mradi wa Kimkakati wa kufua umeme katika bonde la Mto Rufiji.
Waziri Jafo amesema haya leo mara baada kufanya ziara ya kikazi
ya kukagua uzingatiaji wa masharti yaliyowekwa katika cheti cha Tathmini ya
Athari kwa mazingira kinachotolewa na Ofisi yake.
Amesema ameridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Mhandisi Mkazi
wa TEKU John Mageni kuhusu hatma ya mashimo yanayochimbwa kwa ajili ya
upatikanaji wa madini ujenzi ikiwemo mawe, kokoto na mchanga.
"Nnimeridhika na maelezo ya wataalamu wetu kuwa mashimo haya yatatumika kama chanzo cha mazalia ya viumbe hai wa majini baada ya mradi kukamilika, nimefarijika sana" Jafo alisisitiza.
Jafo amemuagiza Mhandisi
Mkazi na wakandarasi kuhakikisha kuwa vyuma chakavu na taka za
kielektroniki zinazozalishwa katika mradi huo zinafuata taratibu za kimazingira na kuuzwa
kwa wafashabiashara wenye vibali vya Serikali vya mazingira ikiwa ni pamoja na
kibali cha ukusanyaji, kibali cha kuhifadhi na kibali cha kusafirisha taka na
kusisitiza kuwa taka zote zinazozalishwa eneo la ujenzi ni lazima kukidhi
matakwa ya kimazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano ma Mazingira Mhe. Selemani Jafo amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka kusimamia kwa ukaribu na kufuatilia ajenda ya mazingira, uhifadhi na usimamaizi wa Mazingira katika ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere.
Akikagua mfumo wa Maji taka katika eneo la ujenzi, Waziri Jafo ameagiza Afisa Mazingira wa Mradi huo kuhakikisha anatunza takwimu za kiasi cha maji taka yanayozalishwa katika eneo hilo.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samwel Mafwenga amesema.ameyapikea maagizo yaliyotolewa na Waziri Jafo kwa Taasisi yake ya kuhakikisha inafuatilia masuala yote ya takwa la kimazingira katika mradi huo. " Tumepokea maelekezo ya Mheshimiwa Waziri na tutaendelea kuusimamia huu mradi mkubwa wa ufuaji umeme katika masuala yoye ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira"
Awali Meneja wa Mradi huo Mhandisi Mkazi John Mageni amesema shughuli zote zinazoendelea zimezingatia takwa na mahitaji ya Sheria ya mazingira kwa mujibu wa cheti cha mazingira walichopewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
Waziri Jafo ametembelea mradi huo wa kufua umeme kwa lengo la kujionea masuala mbalimbali yanayohusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira. Ujenzi huo wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere umefikia asilimia 54 ya utekelezaji kati ya asilimia 59 zilizokusudiwa na unaratajiwa kukamilika tarehe 14/06/2022.
No comments:
Post a Comment