Na Mwashungi Tahir Maelezo Zanzibar. 15-7-2021
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Maji, Nishati ZURA Bihindi Nassor Khatib wamekabidhi hundi ya Millioni ishirini kwa waandaaji wa mbio za marathon yanayotarajiwa kufanyika tarehe 18-7 -2021.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko katika Ukumbi wa ZURA amesema fedha hizo lengo lake kuwazidisha nguvu mashindano hayo ambayo yatahamasisha wazanzibar na kuweza kuibua vipaji kwa washiriki hao.
Amesema mashindano hayo yatawaimarisha mamlaka hiyo kwa kuitangaza na kuboresha huduma zao ikiwemo mafuta, nishati na gesi pamoja na kukuza sekta ya utalii ambapo utazidi kuimarika kwa vile inaingiza pato kubwa kwa Serikali.
Pia amesema ZURA ina kawaida ya kuwasaidia watu wenye mazingira magumu, walemavu wa viungo na wa akili kwa lengo la kuwapa misaada hiyo ili na wao waweze kufarijika kwa kujikimu maisha yao.
Bihindu amesema kwa vile Serikali inathamini michezo ndani ya wao ZURA wana timu ya michezo wa mpira wa miguu na ndani ya mashindano hayo wafanyakazi 18 watashiriki katika mbio hizo za marathon kwa kilomita 5 na 10.
“Michezo ni afya, mashirikiano na kupata kuweza kujuana hivyo na sisi hatuna budi kuunga mkono suala hili na ZURA ipate kujitangaza kwa huduma zao wanazozitoa kwa wananchi”, alisema Mkurugenzi huyo.
Nao waandaaji wa mashindani hayo ya marathon wamefurahishwa sana kwa kupatiwa kiasi cha fedha hizo na wamesema wamepata matumaini makubwa kwa kupata wafadhili na kutokana na nguvu waliyopata wanatarajia na mwakani kuandaa tena mashindano hayo.
Mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 18-7-2021 yatafunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi huko Forodhani na washiriki watakimbia kilomita 5 ,10 na zaidi hadi kumalizikia katika Uwanja wa Amani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment