Na:Lillian Shirima – MAELEZO.
Wadau ya wanamichezo wataendelea kumkumbuka aliyekuwa rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa kwa zawadi ya ujenzi wa Uwanja wa Taifa, sasa Uwanja wa Mkapa,ambao umeleta hamasa katika tasnia ya michezo.
Akiongea na Idara ya Habari-MAELEZO
Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Miundombinu ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge
amesema, wakati taifa linaadhimisha mwaka mmoja wa kumbukizi ya aliyekuwa rais
wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin
William Mkapa wadau wa michezo wataendelea kumkumbuka kutokanaujenzi wa Uwanja
wa Michezo ulioanza kujengwa ulianza kujengwa mwaka 2003 wakati
wa uongozi wake.
‘Tangu kujengwa kwa uwanja huu viwanja
vingine vidogo zaidi ya 9vimejengwa na watu binafsi pamoja na Taasisi.Hii
imewatia moyo wadau mbalimbali kama Azam’.
Aidha amesema, Hayati Mkapa alikuwa
kiongozi mwanamapinduzi,mwenye njozi ya kuona watanzania wanatumia michezo si
kwa ajili ya burudani au kuimarisha afya
pekee bali kuimarisha mshikamano, kuleta umoja wa kitaifa lakini pia
michezo itanyike kwa maendeleo ya taifa, pengine hiyo ilikuwa zawadi ya ndoto
yake kwa watanzania;Ujenzi wa Uwanja wa Michezo.
Akielezea tija itokanayo na uwanja huo
amesema, serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imekuwa
ikishughulika na ustawi wa wananchi hivyo shughuli kubwa zinazofanyika uwanjani
hapo hukusanya watu wenye itikadi tofauti za kisiasa, dini na utaifa ambao
kwahufurahi na kuburudika pamoja.
Hata hivyo amesema, mbali na masuala ya
burudani mechi kubwa au matukio makubwa yanapofanyikahutoafursa kwa vikundi
zaidi ya sita vya vijana vinavyojiandikisha mapema kabla ya tukio kutoa huduma
ya vyakula na vinywaji ndani ya uwanja hukuwajasiriamali wengine wengiwakipata nafasi
ya kufanya biashara mbalimbali nje ya uwanja ambapowatu zaidi ya 5,000
wanakadiriwa kuwepo.
‘Wajasiriamali wengi wanaoishi maeneo
yanayozunguka uwanja na wale waishio jirani hutegemea kujipatia kipato kutokana
na kuwepo kwa Uwanja wa Mkapa hivyo, tunapozungumzia Mkapa tunazungumzia maisha
ya makundi ya watu wanaonufaika na kujishirikisha na masuala ya biashara ndogo
hasa wakazi wa temeke na maeneo mengine’.
Akielezea mabadiliko ya jina la uwanja
huo Nkenyenge amesema, maamuzi aliyofanya Hayati John Pombe Magufuli, rais wa
awamu ya tanokuamua uwanja wa taifa uitwe Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni faraja
kubwa kwa wadau wa michezo kutokana na ukweli kwamba siku zote wananchi watakapoingia
uwanjani au kuangalia matukio yanayoendelea uwanjani hapo kupitia luninga wataendelea
kumkumbuka Mkapa.
Jina la Uwanja wa Mkapalilitangazwa na Hayati John Pombe Magufuli wakati wa
hafla ya kitaifa ya kuuaga mwili wa Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia Julai
24, 2020 Jijini Dar es Salaam.
Uwanja huu wa Mkapa upo katika wilaya ya
Temeke Jijini Dar es Salaam ulianza kujengwa mwaka 2003 ikiwa ni muhula wa pili
wa hayati Benjamin Mkapa madarakani na kumalizika mwaka 2007 ambapo ujenzi wake
ulifanyikakwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na China kama sehemu za programu za kidiplomasia kwa gharama ya dola za
kimarekani Milioni 57.
Wataalam wanatafsiri kuwa, uwanja ni eneo
kubwa lililojengwa kwa wachezaji kucheza na kwa watazamaji kuangalia michezo
mbalimbali, matamasha, na matukio mengine mengi yanayoendelea uwanjani hapo na
kwamba usanifu wa ujenzi wa uwanja unafanywa kwa namna ambayo watazamaji
wanaweza kuona chochote bila kujali upande waliokaa.
Kutokana na kukidhi viwango vyamahitaji
yote ya michezo kimataifa, Uwanja wa Mkapa
umethibitishwa na FIFA pamoja na Shirikisho la Riadha Dunianina unatumika
kwa shughuli nyingi tofauti zikiwemo za kitaifa ingawa mpira wa miguu ni mchezo
unaotumia zaidi uwanja huu.
Ukiwa na uwezo wa kuchukua mashabiki elfu
60, uwanja wa Mkapa ni miongoni mwa viwanja vikubwa Afrika na mkubwa kuliko
yote nchini. Tangu kukamilika kwake michezo mbalimbali imefanyika, mechi za
kirafiki, kitaifa na kimataifa zimefanyika.
Kadhalika, uwanja unatakadiriwa kuchukua
miaka 30 kabla ya kufanyika kwa matengeneza makubwa, hii inatokana na ujenzi
wake kutumia teknolojia ya juu.
Baadhi ya timu kubwa za kimataifa
zilizowahi kucheza katika uwanja huu ni Evaton, Ivorycost, na Brazil na kupitia
timu hizi nchi yetu inajitangaza.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2019 Tanzania
ilikuwa mwenyeji wa finali ya mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana chini ya
umri wa miaka 19na hata ile ya AFCON chini ya 17 ilifanyika ndani ya uwanja wa
Mkapa.
Katika kuenzi mchango wa Hayati Benjamin Mzee aliyesimamia dhana ya uwajibikaji,watanzania tutaendelea kumkumbuka kwa kutujengea uwanja wa michezo wenye miundombinu ambayo haitofautiani na ile iliyojengwa katika nchi zilizoendelea duniani na kupitia michezo tunaimarisha upendo, umoja na mshikamano wa taifa letu.
No comments:
Post a Comment