Habari za Punde

Ufunguzi wa Mkutano wa Wadau Kupitia Sheria.

KATIBU wa Mtandao wa asasi zisizo za Kiserikali Pemba (PACSO) Sifuni Ali Mohamed, akiwakaribisha wadau wa kujadili mapitio ya sheria ya Jumuiya namba 6 ya mwaka 1995, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.
WADAU wa kujadili mapitio ya sheria ya Jumuiya zisizo za kiserikali namba 6 ya mwaka 1995, wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa mkutano huo wa kupitia sheria hiyo, huko katika ukumbi wa kiwanda cha Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.

MRAJIS wa Jumuiya Zisizo za Kiserikali Zanzibar Ahmed Khalid Abdalla, akizunguma na wadau wa kujadili mapitio ya sheria ya Jumuiya namba 6 ya mwaka 1995, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.

MWENYEKITI wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Khadija Bakari Shamte, akifungua mkutano wa siku moja wa wadau wa kujadili mapitio ya sheria ya Jumuiya namba 6 ya mwaka 1995, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Makonyo Wawi Chake Chake Pemba.

(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.