Na: Lillian Shirima – MAELEZO
Ni mwaka mmoja sasa tangu tulipoondokewa na mpendwa wetu Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa T anzania Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Wiliam Mkapa aliyefariki usiku wa kuamkia Julai 24, 2021 Jijini Dar es Salaam
Wakati tunaathimisha kumbukiza ya maisha yake, Wahandisi
Kitainda Michael – Head of Consultancy Services (Mkuu wa Huduma za Ushauri) na
Mohamed Ntunda, Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara TANROADS ni miongoni mwa
wahandisi waliosimamia ujenzi wa Daraja la Rufiji sasa Daraja la Mkapa wameeleza
namna ambavyoHayati Benjamin Mkapa alivyokuwa akifuatilia kwa karibu ujenzi wa
daraja hilokiasi cha kupewa jina la Injinia wa Projekti.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Habari MAELEZO
Jijini Dar es Salaam, Mhandisi Kitainda amesema kwamba, Hayati Rais Mkapa
alikuwa kiongozi asiyechoka kufuatilia jambo lenye maslahi kwa wananchi na kwamba
mara kwa mara alifika eneo la mradi kujua hatua zote za maendeleo ya mradi na
kwamba alipenda kuwasikiliza na kutatua changamoto walizokutana nazo wakati wa
ujenzi.
‘Mkapa alikuwa anatembelea eneo la kazi mara kwa mara
na kila wakati alipofika kuna kitu utajifunza kutoka kwake, alifuatilia kipindi
chote cha ujenzi hadi akaitwaInjinia wa Projekti, alitutoa hofu na kutupa
ujasiri wa kuendelea na kazi hata tulipokwama aliingilia kati na kusaidia na
sisi tulifanya kazi kwa bidii’, alisema Mhandisi ...
Aidha Mhandisi Kaitanda amesema, Hayati Mkapa alikuwa kiongozi aliyebeba maono makubwa,
mwenye kutoa hamasa na matumaini kwa wengine kwa kuwaonesha kitu ambacho
hawakukiona na aliwapa matumaini kwamba hakuna kisichowezekana.
Alitambua kwamba, kwa miaka mingi uchumi katika
mikoa ya kusini mwa nchi ambayo ni Mtwara na Lindi ilikuwa imelala
na kwamba ili kujenga uchumi wa Taifa suala la matumizi ya ardhi halinabudi
kupewa kipaumbele, hivyo alipoingia madarakani alianzisha taasisi nyingi nchini ikiwemo Wakala wa barabara Tanzania
(TANROADS), wahusika wakuu wa ujenzi wa Daraja la Mkapa.
Kabla ya ujenzi wa daraja hilo Mhandisi
Kaitanda ameelezea adha walizokutana nazo wananchi hadi kupoteza maisha ni pamoja na kushindwa kuvuka Mto Rufiji kwenda ng’ambo ya pili
kufuata huduma kutokana na mto huo kujaa maji pamoja na mamba wengi hususan wakati
wa masika.
‘Mara kadhaa kivuko kilikwama kwenye
matope kwa siku zisizotabirika na kusababisha msongamano mkubwa wa magari, wanafunzi walitaabika kwa kukosa
chakula kwa siku kadhaa na hawakujua lini watanasuliwa na kuweza kuendelea na safari’anafafanua Mhandisi Kaitanda
Changamoto
haikuwa hiyo pekee, akina mama wajawazito waliteseka kwa kusoka huduma za
uzazi, wapo waliojifungua njiani, wengine walipoteza maisha yao na ya watoto,
hata vitendo vya ukatili wa kijinsia vilikuwa vinafanyika.
Anasema kwamba, kutokana na kukosekana kwa miundombinu imara hususan
daraja na barabara, suala la usafiri na usafirishaji wa bidhaa katika mikoa hiyo ya kusinililighubikwa
na changamoto lukukina hivyo kusababisha gharama za maisha kuwa juu ambapo
bidhaa kama sukari ilipanda mara tano ya bei iliyokuwepo wakati huo.
‘Hapakuwa na watu wenye maono ya shughuli za
kiuchumi kwa sababu ya kukosa mawasiliano, hakuna masoko, Mfanyakazi
wa serikali akipata uhamisho kwenda mikoa ya kusini utasikia watu wakiuliza
amekosa nini, ilikiwa ni kama adhabu’.
Akielezea historia ya ujenzi wa daraja hilo Mhandisi
Kaitanda alisema, ikumbukwe kwamba mwaka 1974 mikoa ya kusini
ilikumbwa na mafuriko makubwa yaliyoharibumakazi ya watu ambapo Serikali
ililazimika kuhamisha watu waliokuwa wakiishi bondeni kwenda kijiji ambacho
sasa kinaitwa Ikwiriri.
Tukio hilo
lilisababisha Serikali kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya mafuriko ya mto Rufiji
hata ilipofika mwaka 1995 mchakato wa kujenga daraja la kudumu ulipamba moto
ambapo daraja hilo lenye urefu wa mita 970 lilianza
kujengwa kwa gharama
ya fedha za kimarekani dola Milioni 30 ambazo ni fedha za wahisani kutoka OPEC,
Kuwait na Serikali ya Saudia Arabia.
Daraja hilo lililopo mkoa wa Pwani
wilaya ya Ikwiriri na limejengwa kuvuka Mto Rufiji likiunganisha Pwani na Mikoa ya Lindi na
Mtwara ni miongoni mwa alama alizotuchia Hayati Mkapa,lilifunguliwa Agosti 2, 2003.
Tangu
kukamilika kwa ujenzi wake shughuli za kiuchumi na kijamii zimeendelea kukua
kwa ufanisi. Mathalan,usafirishaji wa mizigo na bidhaa zake
umekuwa wa hakika na rahisi hivyo wananchi wananufaika kwa kununua kwa bei
nafuu, uwekezaji mkubwa wa viwanda kama vile Kiwanda cha
Saruji cha Dangote kimetengeneza ajira kwa wakazi wa Mtwara na mikoa mingine.
Kugunduliwa
kwa gesi asilia kumechochea kuongezeka kwa kasi ya ujenzi wa viwanda ambapo
wawekezaji wamewekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo hoteli na taasisi za kifedha.
Kadhalika kukua kwa kilimo cha zao la korosho kumebadilisha maisha ya wakulima
katika mikoa hiyo ya kusini.
Mhandisi
Kitainda anaweka wazi kwamba ataendelea kumkumbuka Hayati Mkapa kwa kuanzisha
Tanroads ambapo mikoa imepewa mamlaka ya kiutendaji hali inayoongeza ufanisi wa
kazi kwenye usimamizi, maamuzi na mgawanyo wa majukumu kiutendaji.
"Kabla
ya TANROADS kazi zote za kihandisi ziliratibiwa na ofisi kuu ya
ujenzi hali iliyosababisha kuzorota kwa kazi, sasa hivi Meneja wa mkoa Tanroads
anaweza kusimamia vizuri barabara na madaraja ya mkoa wake kila siku’
alifafanua zaidi.
Naye
Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara Tanroads Mhandisi Mohamed Ntunda amesema,
licha ya kwamba Mkapa alikuwa na shauku na miradi ya kusini (Mtwara Corridor)
na kwamba mradi wa Daraja la Mkapa ni sehemu ya miradi ya kimkakati.
Amesema, Hayati
Mkapa ni kiongozi aliyesisitiza suala la uwajibikaji katika kazi jambo
lililosababisha ufanisi katika ujenzi wa daraja hili.
"Daraja
halijawahi kufanyiwa matengenezo isipokuwa yale kidogo katika barabara
zinazounganisha daraja hilo"amesema Mhandisi Ntunda.
Hayati Mkapa
ni Kiongozi aliyekuwa na dhamira ya kujenga mazingira yatakayomwezesha
mwananchi kuendesha shughuli zake za kiuchumi kwa faida yake binafsi na
maendeleo ya Taifa. Kumuenzi Hayati Mkapa ni kuwa wazalendo kwa Taifa letu,
kuwajibika katika kazi, na kuweka maslahi ya Taifa mbele.
No comments:
Post a Comment