Habari za Punde

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YATOA ELIMU YA UCHUMI NA FEDHA

Mhasibu Mkuu wa Kitengo cha Pensheni kutoka  Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Scholastica Mafumba, akipata maelezo ya Chuo cha Uhasibu Tanzania, wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Mchumi kutoka Idara ya Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jesca Mugyabuso, akitoa elimu ya Sera kuhusu kodi, wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mchumi wa Idara hiyo, Bw. Mustafa Muhiddin.
Mtaalam wa masuala ya Madeni kutoka Idara ya Madeni ya Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Sepo Seni, akitoa elimu kuhusu deni la Taifa na uhimilivu wake, wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Mchumi kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Joseph Msumule, akitoa ufafanuzi kuhusu usajili wa huduma ndogo ya fedha, wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mkuu na Mchumi Mwandamizi kutoka Idara ya Bajeti, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Raymond Mukwaya na Deusdedit Kaji, wakimsikiliza mwananchi aliyefika katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kupata huduma, wakati wa Maonesho Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Bi. Sarah Goroi, akitoa elimu kuhusu Programu mpya ya Diploma Mobile Applications, inayotarajiwa kuanza kufundishwa kuanzia Oktoba, 2021.

Afisa Manunuzi, Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Bi. Faraja Mgulambwa, akitoa elimu kwa mwananchi aliyeetembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango kupata huduma kuhusu mitiani ya kitaalamu ya ununuzi na usajili wa wataalam, wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), jijini Dar es Salaam.

(Picha na WFM, Dar es Salaam)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.