Habari za Punde

NAIBU WAZIRI CHANDE ASIKILIZA CHANGAMOTO ZA WALIKOKUWA WATUMISHI WA OFISI YAKE ZANZIBAR

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Chande akisikiliza hoja za waliokuwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais hii leo, Tunguu – Zanzibar. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Bw. Sheusi Mburi na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Muungano (Ofisi ya Zanzibar) Bi. Shumbani Ramadhani Tawfiq.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Hamad Chande (kulia) leo 7/07/2021 amekutana na waliokuwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika kikao kazi cha kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Tunguu, Zanzibar na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Bw. Sheusi Mburi na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Muungano (Ofisi ya Zanzibar) Bi. Shumbani Ramadhani Tawfiq

                                                                     Picha na Lulu Mussa 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.