Mkuu wa Taasisi ya Al falasi kutoka (UAE) Ahmad Al-falasi akisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu dhamira yake ya kutaka kusaidia katika sekta ya afya Zanzibar Mkutano uliofanyika Hoteli ya Park Hyatt Shangani Mjini Zanzibar.
Mwandishi wa habari wa ITV Farouk Karim akiuliza maswali katika Mkutano na Mkuu wa taasisi ya Al falasi uliofanyika Hoteli ya Park Hyatt Shangani Mjini Zanzibar.
Mtoto wa Mkuu wa Taasisi ya Al falasi Shaima Ahmad Alfalasi akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wandishi wa habari (kushoto) ni Mke wa Ahmad Al-falasi.
Picha na Makame Mshenga.
Issa
Mzee Maelezo 09/07/2021
Wizara
ya Afya Ustawi wa Jamii,Wazee Jinsia na Watoto inaendelea kushirikiana na
wahisani wa maendeleo katika kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana Nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika majumuisho ya ziara ya kutembelea katika maeneo
mbalimbali ikiwemo vituo vya afya, mkuu wa Taasisi ya Alfalasi Ahmed Alfalasi
amesema taasisi yake itahakikisha inaisaidia Serikali ya Zanzibar katika kuhakikisha
huduma bora za afya zinatolewa Mjini na Vijijini.
Alisema
kuwa katika ziara hiyo wamebaini uhitaji wa matengenezo ya mashine mbalimbali
kwa Hospitali za Zanzibar nakuahidi kuzikarabati ili ziweze kufanya kazi
vizuri.
Alieleza
kuwa tasisi hiyo imepanga mkakati wa kuwaleta mafundi kutoka Nchini Dubai ili
kuzitengeneza mashine hizo pamoja na kuwapa ujuzi mafundi waliopo Zanzibar ili
kuwajengea uwezo wa kuzitengeneza mashine hizo jambo ambalo litasaidia katika
kuleta ufanisi hospitalini.
Aidha
alisema miongoni mwa maeneo yanayohitaji
msaaada ni pamoja na Benki ya Damu
pamoja na wodi ya wazazi ambayo inatarajiwa kupata msaada hivi karibuni.
Akizungumzia
kuhusu suala la msaada wa dawa mkuu huyo alisema atafanya mazungumzo na Wizara ya afya Nchini Dubai
ili kuona namna nzuri ya kuipatia Zanzibar msaada huo.
No comments:
Post a Comment