Habari za Punde

ZATU yaharakisha uundwaji wa Tume ya Walimu Zanzibar

Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) Salim Ali Salim akisoma taarifa kwa Waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu maboresho ya Sekta ya Elimu Zanzibar.


 BAHATI HABIBU   MAELEZO ZANZIBAR          2/7/2021.

 Kuharakishwa kuundwa kwa tume ya Utumishi ya   Walimu Zanzibar na Serkali  ya Mapinduzi ya Zanzibar   kutasaidia kuboresha ufaulu wa wanafunzi wa Skuli za Zanzibar  katika mitihani yao ya kitaifa.


Hayo yamesemwa na  Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) Salim Ali Salim wakati akizungumza na Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Kijangwani Mjini Zanzibar, amesema tume ya utumishi ya Walimu ina umuhimu katika kufikia maendeleo ya Elimu Zanzibar.


Amesema kuundwa kwa tume hiyo  Zanzibar itawasaidia walimu kupanga mikakati  na mbinu bora za kumuandaa Mwanafunzi ya kujifunzia na kuandaa mazingira bora  ya Walimu ya kufundishia.


Aidha ameiomba Serekali kuwashirikisha  wadau wa elimu na walimu kupitia vyama vyao vya ushirika  ikiwemo ZATU wanashiriki  kupanga mipango inayohusu sekta ya Elimu Zanzibar.


Akitolea mfano wa Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika Bajeti ya mwaka 2021/2021 ushirikishwaji ulikuwa mdogo  kwa Chama cha walimu Zanzibar .

Amesema Bajeti hiyo haikuzungumzia  hadhi ya kazi ya uwalimu na maslahi ya walimu jambo ambalo linapelekea walimu kukosa hamasa ya kufundisha na kusababisha matokeo kuwa mabaya.


Akielezea suala la maslahi ya Walimu ni muhimu kupatiwa nyumba za kuishi , kuongozewa mishahara na kupatiwa usafiri wa uhakika ili kuwasaida na hali ngumu wanayopitia hivi sasa  ikiwa ni pamoja na kuchelewa kufika Skuli kwa wakati.


Aidha ameiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  kuhakikisha walimu ambao wanadai stahiki zao ikiwemo malimbikizo ya deni la nauli na likizo , ambapo hadi sasa wanadai posho la nauli kwa miezi 12.


Pia bwana Salim ameiomba  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuandaa mijadala shirikishi itayotoa fursa ya kuonesha njia ya kuboresha ufaulu wa Wanafunzi na kuisaidia Serekali kuandaa mikakati ya kufikia lengo hilo.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.