Habari za Punde

Tamasha la Zuchu Lawapagawisha Wazanzibar. Mcheza Kwao Hutunzwa Zuchu Coming Home na Zantel.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Zantel, Aneth Muga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa tamasha la Zuchu Home Coming na Zantel jana katika viwanja vya Amani Zanzibar.Tamasha hilo lilihusisha wasanii mbalimbali wakiwamo wa Zenjifleva na Bongo Fleva.

Mcheza kwao hutunzwa! hivyo ndivyo unavyoweza kueleza jinsi tamasha la Zuchu Home Coming na Zantel lilivyokonga nyoyo za watu wengi katika Viwanja vya Amani Zanzibar usiku wa jana.

Tamasha hilo liliofanyika jana lilipambwa na wasanii wa muziki kutoka Zanzibar ‘Zenjifleva’ akiwamo Sultan King, Berry black, Cholo na malkia wa mipasho Khadija Kopa.Pia, lilishuhudia wasanii wa Bongo fleva akiwamo Mr.Blue, Lavalava, Mbosso,Chege, Jux,Lulu diva na Queen Darleen.

Moja ya wasanii walioonekana kukonga nyoyo za wengi ni pamoja na mama mzazi wa Zuchu Khadija Kopa ambaye alitumbuiza kwa miondoko ya Taarabu na kupata shangwe kubwa kutoka kwa watu waliokuwapo uwanjani hapo.

Zuchu alianza kwa kutumbuiza nyimbo zake maarufu ikiwamo wimbo wa itawachoma, nisamehe na baadaye kuhitimisha kwa shangwe kubwa alipoimba wimbo wake wa Sukari.

Awali, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Zantel Aneth Muga alisema tamasha hilo pamoja na mambo mengine lililenga kutambua vipaji mbalimbali vya muziki kwa kuwapa wasanii hasa wachanga nafasi ya kuonesha vipaji vyao.

Huu ni mwendelezo wa Kampeni yetu ya Pasua Anga Ki Zantel 4G ambayo inalenga kutoa elimu juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuleta manufaa ya kijamii na kiuchumi.

“Sote tunafahamu kwamba Zuchu ni mtoto na kipaji wa nyumbani kwetu Zanzibar na kupitia tamasha hili Zuchu anarudi nyumbani kwa kutoa burudani ya aina yake hapa Uwanja wa Amani.Pia, kupitia tamasha hili, wanamuziki wa Zenjifleva watapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao ili na wao waweze Kupasua Anga kama ambavyo Zuchu amefanya,” alisema.

Aliongeza kuwa kupitia intaneti ya 4G, unaweza kufanya mambo mengi ambayo yanaweza kubadilisha kabisa dunia yako.Zuchu amekuwa mfano mzuri ambapo kupitia intaneti ameweza kuendeleza kipaji chake kwa kujifunza mambo mbalimbali ya muziki mtandaoni.

Mbali na wasanii tamasha hilo lilihudhuriwa na viongozi kutoka Serikalini akiwamo Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mh.Tabia Mwita,Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.