Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Balozi Mdogo wa Msumbiji Anayefanyia Kazi Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  (kulia)akizungumza na Balozi Mdogo wa Msumbiji anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe.Agostino Abacar Trinta alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi  (kulia) akipokea hati ya utambulisho kutoka kwa  Balozi Mdogo wa Msumbiji anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe.Agostino Abacar Trinta alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kujitambulisha .[Picha na Ikulu.] 04 Aug 2021. 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi  ameahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya  Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Msumbuji.


Dk. Mwinyi ametoa ahadi hiyo leo Ikulu Jijini Zanzibar alipokutana na Balozi Mdogo wa Msumbiji aliopo Zanzibar Agostino Abacar Trinta aliefika Ikulu kujitambulisha.


Amesema nchi hizo zimekuwa na uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu, hali inayotoa fursa kwa Wazanzibari  wengi kupata fursa ya kuishi na kufanyakazi mbali mbali nchini  humo, hususan eneo al Kaskazini mwa nchi hiyo.


Aidha, alisema nchi hizo zimekuwa zikiunganishwa kupitia Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo Rais wa nchi hiyo Felipe Nyusi ndie Mwenyekiti wake  


Nae, Balozi Mdogo wa Msumbiji   aliopo Zanzibar Agostino Abacar Trinta, aliipongeza Zanzibar kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi mbili hizo, kwa maslahi ya wananchi wa pande mbili pamoja na misaada mbali mbali inayotoa kwa nchi yake.


Balozi Trinta amemtakia afya nje na maisha marefu Rais wa Zanzibar na Mwenyektii wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, yeye pamoja na familia yake.


Aidha, Balozi huyo alitumia fursa hiyo kuwasilisha barua maalum ya salamu kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji Felipe Nyusi pamoja na barua ya Utambulisho.


Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822  

 E-mail: abdya062@gmail.com.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.