Habari za Punde

Serikali Imetoa Bilioni 1.2. Kwa Ajili ya Mradi wa Mkubwa wa Maji Vijiji vya Kata ya Sigiri.Wilayani Nzega.

Mkuu wa wilaya ya Nzega Acp Advera Bulimba akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Kata ya Sigiri Wilaya ya Nzega.

Na Lucas Raphael,Tabora

Serikali imetoa shilingi bilioni 1.2 kwa ajili ya mrari mkubwa wa maji katika vijiji vinavyozunguka kata ya sigiri wilaya ya Nzega mkoa Tabora.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu mratibu wa Taifa wa Mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya Tanzania (LDFS)kutoka ofisi ya makamu wa Rais Mazingira,Yobu Kiungo wakati akikabidhi hati za kimila kwa wananchi wa kata ya Sigili.

Alisema kwamba fedha hizo zitakutumika katika kazi mbalimbali za kutambua na kufanya upembuzi yakinifu kwa vyanzo vya maji na Teknolojia  itakayotumika katika uvunaji wa maji.
Alisema kwamba hatua nyingine ni uchimbaji wa  malambo 3 ,Visima virefu 6 na Bwawa 1 ili kuwapunguzia tatizo la maji ya wananchi na mifugo.

Kiungo alisema kwamba wananchi wanatakiwa kupata mafunzo ya kusimamia mashamba Darasa kwa wawezeshaji kutoka katika vikundi 21 vyenye washiriki 111 walipewa mafunzo ya kilimo,misitu,mifugo na jinsia.

Alisema kuwa  vijiji ambavyo vitakavyonufaika na mradi huo ni Sigili ,Bulunde,Bulambuka,Lyamalangwa na Iboja.

Awali mratibu wa maradi huo wilaya ya Nzega Hassani Mtomela alisema kwamba wanmakusudia kutoa mafunzo ya shamba darasa kwa wakulima kuhusu kilimo hifadhi na mbinu bora za kilimo rafiki kwa mazingira.

Alisema kwamba mafunzo hayo yataenda sambamba na kuwasaidia wakulima katika upatikanaji wa mbinu bora za kilimo na pembejeo kwa wakulima katika mashamba darasa yatayoanzishwa.

Alisema kwamba wakulima, wafugaji na wananchi watapaitiwa mbinu rahisi ya uvunaji maji na ukarabati au uchimbaji wa mabwawa ya kuhifadhi maji kwa ajili ya kilimo, mifugo na matumizi ya jamii.

Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora ni moja kati ya halmashauri tano za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazotekeleza mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame Tanzania.
Naye meneja kanda ya kati Suzana Mapunda kutoka Tume ya Taifa ya Mipango na Usimamizi Bora wa Ardhi alisema kwamba kwa kushirikiana na Tume ya Mipango Ardhi ya Zanzibar watawezesha kazi   ya kuwajengea uwezo na kuwashirikisha katika upangaji wa matumizi ya bora ya ardhi.
Hata Hivyo Mkuu Wa Wilaya Ya Nzega mkoani hapa ACP Advera Bulimba amesema kwamba Serikali inatarajia kuchimba visima sita (6) na kukarabati mabwawa madogo matatu (3) na kuchimba bwawa jipya moja (1).

Alisema kwamba yYote haya ya tafanyika katika Kata ya Sigili kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, mifugo na kilimo.

Alisema kwamba mpaka sasa Serikali imeshatoa jumla ya shilingi 261,004,590/= kwa ajili ya uchimbaji wa visima sita (6) katika vijiji vya Bulambuka, Lyamalagwa na Bulende.

Aidha alisesisitiza kwamba  kwa mwaka huu wa fedha Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ukarabati na uchimbaji wa mabwawa.

Aliongeza kusema kwa kuipongeza  Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuona umuhimu wa kuleta mradi huu,Naipongeza Tume ya mipango ya matumizi Bora ya ardhi, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.

Bila kuacha  Serikali za vijiji na wananchi kwa ujumla kwa ushiriki  mkubwa nawadhati katika kufanikisha shughuli hii, twende tukatekeleze tulicho kipanga kwa ajili ya  maendeleo    yetu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.