Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Akagua Ujenzi wa Mradi wa Reli ya SGR.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu  ujenzi wa karakana kuu ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) , Masanja Kadogosa  (kushoto) wakati alipokagua ujenzi wa  karakana hiyo kwenye eneo la Kwala mkoani Pwani, Septemba 12, 2021. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu  ujenzi wa karakana kuu ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) , Masanja Kadogosa  (kushoto) wakati alipokagua ujenzi wa  karakana hiyo kwenye eneo la Kwala mkoani Pwani. 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika  la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa (kushoto) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR katika Stesheni Kuu ya Dar es salaam
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya treni maalum ya wahandisi wa kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya kisasa (SGR) wakati alipokagua ujenzi wa reli hiyo kutoka Dar es salaam hadi Kilosa mkoani Morogoro, Septemba 12, 2021.  Katikati ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamriho na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa karakana kuu ya Reli ya Kisasa (SGR) inayojengwa katika eneo la  Kwala mkoani Pwani  wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa reli hiyo kuanzia Stesheni Kuu ya Dar es salaam hadi Kilosa mkoani Morogoro, Septemba 12, 2021. Wa nne kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamriho na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuka kutoka kwenye treni ya wahandisi wanaojenga Reli ya Kisasa (SGR) wakati alipofika kwenye eneo la Kwala Mkoani Pwani akiwa katika ziara ya kukagua mendeleo ya ujenzi wa reli hiyo kutoka Dr es salaam hadi Kilosa mkoani Morogoro.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mkono kuwaaga wafanyakazi wa Kampuni ya Yapi Merkezi baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa karakana  kuu ya Reli ya Kisasa  (SGR) kwenye eneo la Kwala mkoani Pwani, Septemba 12, 2021. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa  Pwani, Abubakar Kunenge.
 (Piacha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.