VIONGOZI wa Sherikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Kulia
ni Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Micheweni Mgeni Khatib Yahya, akifuatilia kwa makini Maadhimisho ya siku ya
Bahari duniani ambapo Kitaifa Tanzania yamefanyika Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
AFISA Mdhamini Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na
Uchukuzi Pemba Ibrahim Saleh Juma, akitoa salamu za katibu mkuu wa Wizara hiyo
wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Bahari Duniani kitaifa Tanzania yamefanyika
Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,
PEMBA)
MKURUGENZI wa Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya
Ujenzi na Uchukuzi SMT Stella Katondo akitoa salamu za katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, wakati wa Maadhimisho ya siku ya bahari duniani kitaifa Tnazania
yamefanyika Kisiwani Pemba.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud
akitoa salamu za wananchi wa mikoa miwili ya Pemba, wakati wa maadhimisho ya
siku ya Bahari Duniani, kitaifa Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika Kisiwani
Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment