Habari za Punde

Mama aliyetelekeza mtoto wa miezi minane akamatwa

Mkurugenzi Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee Abdulla Saleh Omar, (kulia) akiwaeleza Waandishi wa habari tukio la kutupwa Mtoto wa Miezi minane , huko Ofisini kwake Welezo Mjini Zanzibar.
Afisa Ustawi katika Kitengo cha Hifadhi ya Mtoto,Ramadhan Mohammed Ramadhan, (kushoto) akiwaelezea Waandishi wa habari  hatuwa walizochukuwa baada ya kumkamata  Doris Moses Mazigu Mkaazi wa Kianga (hayupo pichani) ambae amemtelekeza mtoto akiwa na miezi minane, huko Ofisini kwake Welezo Mjini Zanzibar.
Sheha wa Shehia ya Mbuzini, Ndagula Hassan Juma, (aliyevaa mtandio wa Njano) akielezea Waandishi wa habari  jinsi walivyomkamata  Doris Moses Mazigu, ambae amemtelekeza mtoto akiwa na miezi minane, na kumpeleka kunakohusika kwa hatua zaidi.

 Doris Moses Mazigu Mkaazi wa Kianga Wilaya ya Magharibi “A” (wa kwanza kulia) akiwaeleza Waandishi wa habari  chanzo cha kumtelekeza mtoto wake akiwa na miezi minane.

Picha na Maryam Kidiko / Maelezo Zanzibar

Pili Ali    -  Maelezo       

Idara ya Ustawi wa Jamii Zanzibar imemkamata Mama Mzazi wa mtoto aliyetelekeza mwenye umri wa miezi minane  kwa kumuacha nyumbani bila ya kumpa huduma yoyote huko maeneo ya Kianga Wilaya Magharibi “A” Unguja.

Mama huyo anaejulikana kwa jina la Dorice Moses Mazigu mwenye umri wa miaka 27 alikamatwa leo huko Mbuzini  Wilaya ya Magharibi A katika kumbi za starehe  na Idara ya Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na masheha wa shehia ya Kianga  na Mbuzini.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupatikana mama huyo  huko Welezo Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamiii na Wazee Abdalla Saleh Omar huko Ofisini kwake, amesema Mama huyo yuko chini ya uangalizi wa vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua za kisheria.  

Nae Afisa Ustawi wa Jamii katika kitengo cha Hifadhi ya Mtoto Ramadhan Mohamed Ramadhan amesema hali ya mtoto huyo imedhoofika kutokana na kukosa huduma za mama na uangalizi mazuri.

Ameeleza kuwa mtoto huyo anapatiwa huduma  katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja  kwa matibabu ambae anasumbuliwa na vidonda pamoja na tatizo la utapia mlo yuko chini Idara ya Ustawi wa Jamii kwa huduma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.