Habari za Punde

Mchezo wa Ngao ya Jamii Uzinduzi wa Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya Mafunzo na KMKM Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan. Mafunzo Imeshindia Mchezo huo Bao 2-.1

Warembo maalum walioandaliwa kubeba Ngao ya Jamii wakati wa mchezo wa Ufunguzi wa Ligi Kuu ya Zanzibar  Kati ya Mafunzo na KMKM Mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.Timu ya Mafunzo imeshinda mchezo huo kwa bao 2-1. 
Waamuzi na Wachezaji wa Timu ya KMKM na Mafunzo wakiwa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kabla ya kuaza kwa mchezo wa Ngao ya Jamii. kwa ajili ya Ufunguzi wa Ligi Kuu ya Zanzibar kwa msimu wa mwaka 2021 /2022. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akimkabidhi Ngao ya Jamii Kepteni wa Timu ya Mafunzo baada ya kushinda mchezo huo dhidi ya KMKM mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar Timu ya Mafunzo imeshinda bao.2-1. 

Classic Game ya Mabingwa imepingwa kwenye Dimba la Amani,Vilabu vyote wamejiandaa vizuri na wapo tayarii kuanza msimu mpya wa Ligi 2021_2022

Mafunzo walikuwa vizurii zaidi kwenye idara zote kulinganisha na wapinzani wao na nidham yao kwa wapinzani ilikuwa juu, Kmkm walimkosa kiungo wao fundi Moha'd Said "Messi" labda ilichangio kupungua kwa kasi yao zaidi walipofika kwenye robo ya 3 (M 25 _ 30) kutoka kwenye lango la wapinzani

Kmkm walijiamini kupitiliza ni kama walikuja kushinda tu Mechi bila ya kupambana na ndio sababu Magoli waliofungwa yalitokana na Makosa ya kizembe waliofanya Back line yao na safu ya kiungo

 Goli la kwanza walifanya watch Making (Kukaba kwa macho) matokeo yake "Udindi" anakuja kufunga Goli akiwa free haider up

Goli la Pili Samir Yahya anapiga Pasi mkaa kwa Kokoi anainasa Fahad na kuanzisha movement,Pressing ilofanywa  na Kokoi & Samir baada ya kupoteza mpira ilikuwa ya ovyo sana kwa Dakika zile,Mourinho na Diego Simeone huna cha kuwambia wanamini Red Card ni halali yako

Mafunzo walifanya kosa 1 kubwa ambalo nao liliwagarimu ni pale walipozembea kwa kuiamini Offside trick lakini Abrahmani "Chinga" alikuwa mjanja zaidi yao na akaitokea Cross ya Haji Mwinyi  kuandika bao la kusawazisha

V.I.P STAGE

* Saidi Mussa "Udindi" kimo chake na kazi anayoifanya ni vitu vya kushangaza sana.

* Ibra & Makame wote walichagua kuwa viongozi kwenye safu ya ulinzi kmkm

* Rashid Abdallah "GASKA" amefunga Goli la kideo sana. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.