Habari za Punde

Tusiwe na muhali kutoa ushahidi kesi za udhalilishaji wa kingono - Wito

Baadhi ya  washiriki wa mafunzo ya Udhalilishaji wa kingono wakiwa wamekaa makundi kwa ajili ya kufanya kazi ya pamoja baada ya kupatiwa Mafunzo hayo yaliyofanyika Ukumbi wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Baadhi ya  washiriki wa mafunzo ya Udhalilishaji wa kingono wakiwa wamekaa makundi kwa ajili ya kufanya kazi ya pamoja baada ya kupatiwa Mafunzo hayo yaliyofanyika Ukumbi wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud Juma akitoa ufafanuzi juu ya Udhalilishaji wa kingono wakati wa Mafunzo hayo huko Ukumbi wa watu wenye Ulemavu kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mkufunzi Fatma Ali Haji  akitoa mafunzo ya Udhalilishaji wa kingono yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) yaliyofanyika Ukumbi wa watu wenye Ulemavu Mjini Zanzibar.

Picha Na Maryam Kidiko / Habari Maelezo Zanzibar

Na Rahma Khamis - Maelezo              

Jamii  imeshauriwa kuacha muhali katika kutoa ushahidi wa kesi za udhalilishaji na   kuwapatia  elimu ya udhalilishaji wa kingono  watoto  ili kutokomeza vitendo hivyo katika jamii.

Ushauri huo umetolewa na Mkufunzi kutoka  Jumuiya  ya Utetezi  wa watu wenye kutendewa vitendo vya udhalilishaji wa kingono (ZANEWCA), Fatma Ali Haji  wakatoa kitoa mafunzo  kuhusu udhalilishaji wa kingono, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Umoja wa Watu wenye  Ulemavu Kikwajuni Zanzibar.

Amesema endapo watoto watapatiwa elimu ya udhalilishaji watapata muamko na uelewa juu ya namna ya kuepuka kufanyiwa vitendo hivyo.

Alieleza kuwa, ipo haja kwa wazazi na walezi kuwahamasisha vijana wao na kuacha muhali ili kuepusha athari zinazotokana na udhalilishaji kwani imekua ni kikwanzo kwa wanawake na  watoto.

Amesema watoto nao wana haki kama watu wengine hivyo ni wajibu kuwapatia haki zao za kimsingi ikiwemo kupatiwa afya na ulinzi kwani akikutwa na jambo hilo hatua ya awali ni kufikishwa katika  kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.

Aidha amefahamisha kuwa vitendo vya udhalilishaji wa kingono havitokei mbali kwani huhusisha familia au watu wa karibu hivyo  kuna haja kwa jamii kuacha kuwaficha watu na badala yake kuwa mstari wa mbele ili kitokomeza vitendo hivyo.

“kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanajamii kuwa na uwoga wa kutoa ushahidi endapo vitendo hivyo vimefanyika katika familia jambo hili si sahihi, ni lazima mtuhumiwa apelekwe kunakohusika ili tutokomeze vitendo hivi” alisema mkufunzi huyo.

Mkufunzi Fatma amewataka  wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao hasa wenyeulemavu kuweza kuwagundua mapema endapo watafanyiwa vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkurenzi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar Jamila Mahmoud Juma amesema kuwa sharia inataka mtoto ahifadhiwe kwani anapofanyiwa kitendo cha udhalilishaji wa kingono huathirika kiakili  hivyo ni wajibu wa kumlinda na kumtetea mtoto huyo ili aweze kupata haki yake ya elimu.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa kesi nyingi za udhalilishaji wa kingono hazifikii mwisho kutokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu vitendo hivyo.

Aidha wamewataka wanajamii kuwa tayari kutoa ushahidi katika kesi ili watoto waweze kukingwa na vitendo hivyo  na kuacha kuwalaza pamoja watoto wao hata ikiwa wote jinsia moja

Mafunzo hayo  yamewashirikisha taasisi mbalimbali ikiwemo wanaharakati wa maswala ya udhalilishaji, wanasheria na waandishi wa habari. 


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.