Habari za Punde

Walimu wahimizwa kuelimisha majanga na matatizo yaliopo nchini

 Na Maulid Yussuf WEMA

ZANZIBAR

Maafisa Elimu Wilaya pamoja na Walimu wakuu  wametakiwa kuwahimiza  Walimu wanapoingia kusomesha darasani kuzungumzia majanga na matatizo yaliopo nchini kwa kuwaelimisha Wanafunzi ili waweze kujikinga na kukabiliana nayo wakati yatakapowatokezea.

Hayo yameelezwa na washiriki wa kuchangia Ripoti ya ufuatiliaji wa Mafunzo ya Stadi za maisha, iliyowasilishwa na Maafisa kutoka Kitengo cha Elimu Mjumuisho na Stadi za Maisha, katika ukumbi wa Kituo cha Walimu TC Kiembesamaki Mjini Unguja.

Wamesema kumekuwa kukijitokeza matatizo mbalimbali nchini yakiwemo ya udhalilishaji, maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi pamoja na Janga la korona ambapo Wanafunzi wakipewa elimu ya majanga hayo wataweza kujikinga pamoja na kujua namna ya kukabiliana nayo.

Aidha wamesema pia kuna umuhimu wa kupewa elimu kwa jamii juu ya stadi za maisha na kuwafundisha watoto suala zima la ujasiri na kujihami wakati wanapopatwa na majanga mbalimbali hasa ya udhalikishaji.

Akiwasilisha ripoti  ya ufuatiliaji wa mafunzo ya Stadi za maisha, Mkuu wa Seksheni ya Stadi za maisha  kutoka Kitengo cha Elimu Mjumuisho na Stadi za Maisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi Fatma Mbarak Hashim amesema utafiti huo umeshirikisha Skuli 24 ambapo Skuki 14 kutoka Unguja na Skuli 10 kutoka Pemba.

Amesema matokeo ya utafiti huo umebaini kuwepo mabadiliko chanya baada ya kupata mafunzo hayo, ikiwemo Wanafunzi kupunguza kuranda ovyo wakati wa Skuli, kuripoti kwa Walimu wao kuhusu matukio ya udhalilishaji,  kupungua kwa kesi za kujamiiana na utoro, pamoja na kuwafuata Walimu wao kwa kupata ushauri.


Hata hivyo amesema ripoti imebaini kwa kujitokeza matukio yasiyo ya kawaida ikiwemo udhalilishaji wa Mwanafunzi wa kiume wa darasa la tatu kuchukuliwa na Wanafunzi wenzake na kumchezea sehemu zake za siri, pia Mwanafunzi kuchukuliwa na mtu asiejuilikana na kupelekea kutokea taharuki, pamoja na matukio ya kulawitiana miongoni mwa Wanafunzi.

Hata hivyo bi Fatma, amesema Kitengo cha Elimu Mjumuisho na Stadi za Maisha kimepanga kuendeleza mafunzo hayo kwa Skuli nyengine ambazo hazikuwahi kushirikishwa na katika awamu iliyopita kuanzia ngazi ya maandalizi, msingi na Sekondari ili kuhakikisha Elimj ya Stadi za maisha inawafikia watoto na kuweza kupunguza matatizo ya udhalilishaji nchini.

Mapema akifungua Mkutano huo, Afisa Mafunzo kutoka Idara ya Mafunzo ya Ualimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, mwalimu Mohammed Ali Mohammed UGODA,  amesema lenco la kufanywa utafiti huo ni kuangalia kwa namna gani Walimu wameifikisha Taaluma waliyopatiwa ya Stadi za maisha kwa Wanafunzi.

Pia kujua Wanafunzi wamejifunza kwa kiasi gani na namna wanavyoyafanyia kazi mafunzo hayo ya afya uzazi, Stadi za maisha pamoja na namna ya kujikinga vitendo vya udhalilishaji na maambukizi mapya virusi vya Ukimwi.

Mkutano huo wa siku moja wa kuchangia ripoti ya ufuatiliaji aa mafunzi ya Stadi za Maisha,  umewashirikisha Walimu wakuu, Maafisa Elimu Wilaya pamoja na baadhi ya washauri wa Elimu Mjumuisho kutoka Vituo vya Walimu TC.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.