Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Aendelea na Ziara Yake Wilayani Lindi.

Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Benard Membe (katikati), Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Lindi, Athumani Seif  (kulia) na Mkuu wa wilaya Mstaafu, Naaz Mangochi wakifurahia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza na wananchi katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mnara katika jimbo la Mtama, mkoa wa Lindi, Oktoba 5, 2021.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama michoro ya ujenzi wa mradi wa maji wa Mitwero, Mkwaya na Kitunda wilayani Lindi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio  kuhusu maandalizi ya ujenzi wa mradi wa LNG ( mradi wa kusindika gesi kuwa kimiminika ) katika eneo la Likong’o Manispaa ya Lindi wakati alipotembelea eneo hilo akiwa katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Lindi,

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Bruno Ngonyani wakati alipotembelea hospitali ya Nyangao katika Jimbo la Mtama
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Mnara iliyopo Rondo  katika Jimbo la Mtama Mkoani Lindi, Oktoba 5, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.