Wananchi wakiendelea na mazoezi kabla ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika leo Novemba 06, 2021 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Wananchi wakiendelea na mazoezi kabla ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika leo Novemba 06, 2021 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akikata utepe kwenye kitabu ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Kuzuia na kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika leo Novemba 06, 2021 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Timoth Wananji akimkaribisha Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul (wa kwanza kulia aliyevaa jaketi) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika leo Novemba 06, 2021 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mhe. John Mongela akiongea wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya
kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika leo Novemba 06, 2021
katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Naibu Waziri wa
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul akiongea na wananchi (hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa tamasha la michezo katika maadhimisho ya wiki ya
kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza uliofanyika leo Novemba 06, 2021 katika
uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Na Eleuteri Mangi, WUSM, Arusha
Watanzania wamehimizwa
kufanya mazoezi ili kuimarisha afya za miili yao na kuepukana na ongezeko kubwa
la magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa tishio kubwa duniani kote.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul kwa niaba ya
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa wakati wa uzinduzi wa
tamasha la michezo katika maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa
yasiyoambukiza uliofanyika Novemba 06, 2021 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini
Arusha.
“Nipende kuipongeza
sana Wizara ya Afya na wadau wengi kwa kutekeleza na kunialika kuja kufungua
maadhimisho haya ya tatu, kwani michezo ni afya na inasaidia kuimarisha
mahusiano kati ya mtu na mtu au kati ya taasisi au jumuiya moja na nyingine
hivyo kufanya michezo ndani ya jamii kuwa ni ya manufaa makubwa” amesema Mhe.
Gekul.
Naibu Waziri Gekul
amesema kuwa tamasha hilo ni utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kuzuia na
kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza ambao ulizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri
wa Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mwezi Novemba mwaka 2019 ili
kuongeza kasi ya udhibiti wa Magonjwa Yasiyoambukiza.
Mhe. Gekul
amewakumbusha Watanzania kuwa Mhe. Rais kipindi akiwa Makamu wa Rais alizindua
utaratibu wa kufanya mazoezi ya pamoja kila
Jumamosi ya pili ya Mwezi hatua ambayo imesaidia kuongeza vikundi vya
mazoezi ya pamoja katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Ili kuendelea kutekeleza
agizo hilo, Naibu Waziri Gekul ametoa rai kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee
kuwahamasisha uundwaji wa vikundi vya
mazoezi ya pamoja na kuwapongeza wananchi kwa mwitikio wa kufanya mazoezi
katika maeneo yao.
Aidha, tamasha hilo
ni uelekezaji agizo la Watanzania kuadhimisha wiki ya Pili ya Kila Mwezi
Novemba ambayo imetengwa maalum ya Kitaifa ya kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza
hatua ambayoinasaidia kujikita zaidi katika wiki hiyo kutoa elimu ya afya
inayohusu magonjwa haya ambayo yamekuwa tishio la ustawi kwa jamii yetu.
Katika hatua nyingine
Mhe. Gekul amewasisitiza viongozi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Ardhi kusimamia mamlaka za Serikali za mitaa
kuhakikisha zinaweka mazingira bora ya watu kufanya mazoezi kwa kuendelea
kutenga viwanja vya michezo na kuzuia uuzaji wa maeneo ya wazi hususani viwanja
vya michezo pamoja na kuboresha barabara za waenda kwa miguu na baiskeli ili
kuhamasisha watu kutembea na kuongeza usalama kwa watu wanaofanya mazoezi.
Akimkaribisha mgeni
rasmi kufungua tamasha hilo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk. Silvia Mamkwe amesema
mgonjwa yasiyoambukiza yamekuwa tishio nchini na duniani kote, hivyo mazoezi ni
dawa na tiba kwa afya za wananchi.
“Magonjwa
yasiyoambukiza yamekuwa tishio sio tu kwenye jamii yetu, bali ulimwenguni kote
na taswira ya magonjwa hayo imeendelea kuongezeka siku hadi siku” amesema
Mganga huyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Takwimu za Shirika la
Afya Duniani za Mwaka 2016 ambazo zinaonesha kuwa Magonjwa yasiyoambukiza
yanachangia zaidi ya vifo milioni 41, ambayo ni sawa na asilimia 71 ya vifo
vyote.
Kwa upande wa Tanzania
magonjwa hayo yalikuwa yanachangia asilimia 20 tu miaka ya 90, ilifikia
asilimia 33 mwaka 2016, na kwa sasa inakadiriwa yanaweza kufikia hadi asilimia
40 katika baadhi ya maeneo nchini.
Hali hiyo inatia hofu
kuwa katika jamii zetu magonjwa hayo yanaanza mapema zaidi na hivyo kuzorotesha
nguvu kazi na kusababisha vifo katika umri chini ya miaka 60.
Hali hiyo imemlazimu
Naibu Waziri Gekul kusisitiza kila mtu kuchukua hatua za kujikinga na magonjwa
yasiyoambukiza kwakkuzingatia ulaji unaofaa kwa kula mlo kamili, ulaji wa
matunda na mboga mboga za kutosha, kuepuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta
mengi, kuepuka kula vyakula vyenye chumvi nyingi, na kuepuka ulaji wa vyakula
na vinjywaji vyenye sukari nyingi.
Hatua nyingine ni kufanya
mazoezi ya mwili, na kushughulisha mwili, na kuepuka msongo wa mawazo, kupunguza
au kuacha matumizi ya pombe, kuepuka matumizi ya tumbaku na bidhaa zake na
kuacha kabisa matumizi ya dawa za kulevya, kuanza kufanya uchunguzi wa afya
angalau mara moja kwa mwaka hususani kwa watu wenye umri mkubwa wa zaidi ya
miaka 40 pamoja na kuzingatia matumizi sahihi ya barabara na vyombo vya moto
kama gari na pikipiki ili kuepuka ajali za barabarani.
Naye Mkuu wa Mkoa huo
John Mongela amemhakikishia Mgeni rasmi kuwa mkoa huo upo mstari wa mbele
kutekeleza maagizo ya viongozi wa kitaifa kwa vitendo hasa kufanya mazoezi kwa
ajili ya afya ambapo wakazi wa mkoa huo kufanya mazoezi kila siku ni moja ya
jumkumu lao la kila siku.
Vile vile katika tamasha
hilo, Watanzania wakaazi wa Jiji la Arusha wamekumbushwa na wamehimizwa kunapata
chanjo za UVIKO-19 hasa wale ambao hawajachanja ili kujikinga ugonjwa na kuendelea
kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo, kutoa kuelimu na kuhamasishana umuhimu
wa kuepuka misongamano isiyo ya lazima, kuendelea kutumia barakoa, kunawa na
sabuni na maji tiririka.
Maadhimisho ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza yanafanyika kuanzia Novemba 06 hadi 13, 2021 yakiongozwa na kauli mbiu ya inayowasisitiza “Badili Mtindo wa Maisha, Boresha Afya” kwa lengo la kuitaka jamii ya watanzania na wadau wote kushirikiana katika kubadili mtindo wa maisha ili kuwa na afya bora na yenye kuleta tija kwa Taifa letu.
No comments:
Post a Comment