Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi azindua jengo la Hospitali ya Maradhi ya Akili Kidongochekundu

MUONEKANO wa Jengo la Hospitali ya Maradhi ya Akili Kidongochekundu Zanzibar,lililofungunguliwa leo 18-11-2021 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Mradi wa Jengo la Hospitali ya Maradhi ya Akili Kidongochekundu Zanzibar akiwa na  Mfadhili wa Mradi wa ujenzi huo.Bw.Trond Mohn,  Mradi huo umefadhiliwa kupitia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland Nchini Norway na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Hospitali hiyo Kidongochekundu leo 18-11-2021.(Picha na Ikulu) 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kulifungua Jengo la Hospitali ya Maradhi ya Akili Kidongochekundu Jijini Zanzibar akiwa nan a Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Mhe. Nassor Ahmed Mazrui  na Wafadhili wa Mradi huo Bw. Trond Mohn na Mkewe. Mradi huo umefadhiliwa kupitia Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland Nchini Norway na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea jengo la Watoto la Maradhi ya Akili katika Hospitali ya Kidogochekundi Zanzibar baada ya Kuyazindua leo 18-11-2021.yaliojengwa kwa Ufadhili kupitia Chuo Kikuu cha Haukeland Norway na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mtaalam wa Maabara wa Hospitali ya Maradhi ya Akili Kidongochekundu baada kuzindua majengo hayo yaliojengwa kwa ufadhili kupitia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Chuo Kikuu cha Haukeland cha Nchini Norway, (kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto.Mhe. Nassor Mazrui, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Mustafa Idrisa Kitwana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland Nchini Norway Bi. Randi –Luise.(Picha na Ikulu)
MBUNGE wa Jimbo la Jangombe Zanzibar Mhe.Ali Hassan Omar akiwa na Wananchi wa Jimbo lake wakihudhuria hafla ya Ufunguzi wa Jengo la Hospitali ya Maradhi ya Akili Kidongochekundu Jijini Zanzibar iliyojengwa kwa ufadhili wa Chuo Kikuu cha Haukeland Nchini Norway na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui, akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, kuzungumza na Wananchi, wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Jengo la Hospitali ya Maradhi ya Akili Kidongochekundi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wageni waalikwa wakifuatilia hafla ya Ufunguzi wa Mradi wa Jengo la Hospitali ya Maradhi ya Akili Zanzibar, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Hospitali hiyo Kidongochekundi leo 18-11-2021.(Picha na Ikulu)
WAFADHILI wa Mradi wa Ujenzi wa Majengo ya Hospitali ya Maradhi ya Akili Zanzibar Bw.Trrond Mohn na Bi.Randi-Luise, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia katika hafla hiyo ya ufunguzi .(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuhutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Hospitali ya Maradhi ya Akili Kidongochekundu Zanziubar, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la ufunguzi wa jengo hilo leo 18-11-2021, lililojengwa kwa ufadhili kupitia Chuo Kikuu cha Haukeland cha Nchini Norway na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Mfadhili wa Hospitali ya Maradhi ya Akili Kidongochekundu Bw. Trond Mohn akiwa na mkewe, baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa majengo ya Hospitali hiyo leo 18-11-2021.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.