Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba
Ndaki (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Desert Cold Store kutoka
Oman, Dkt. Munawar Pardhan alipokutana
na Wawekezaji kutoka nchini Oman jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba
Ndaki (katikati) akibadilishana mawazo na sehemu ya Wawekezaji waliomtembelea
ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Desert Cold Store kutoka Oman, Dkt. Munawar Pardhan.
Na Mbaraka Kambona,
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema Wizara yake itaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowavutia wawekezaji katika Sekta ya Mifugo ili kukuza thamani ya mifugo na kupandisha kipato cha wafugaji hapa nchini.
Ndaki aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
alipokutana na Wawekezaji kutoka nchini Oman ambao wameonesha nia ya
kufanyabiashara ya kununua mifugo na
nyama hapa nchini na kuuza nchini Oman.
"Tunaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa kadri iwezekanavyo ili muweze kufanya
hiyo biashara na nchi yetu," Ndaki aliwaeleza wawekezaji hao
Alisema kuwa nchi ikipata wawekezaji kutoka nje kama wao ni
jambo jema kwa sababu kupitia wao wafugaji watapata kipato kizuri, lakini pia
itapandisha thamani ya mifugo nchini.
"Tukipata soko la kwenu litasababisha wafugaji wetu
ambao wengi wao kipato chao kipo chini kiweze kupanda, sisi tutafanya kila
linalowezekana ili biashara hii mnayotaka kuifanya iweze kufanikiwa,"
alisistiza
Awali, Mkurugenzi wa Kampuni ya Desert Cold Store kutoka
Oman, Dkt. Munawar Pardhan alisema lengo lao ni kufanya biashara ya mifugo na
nyama, huku akisema kuwa wakifanikiwa itakuwa ni fursa kubwa ya kiuchumi baina
ya nchi hizo mbili.
"Tumekuja hapa Tanzania kujua taratibu za kufuata ili
tuweze kufanya biashara ya mifugo na nyama kutoka hapa na kwenda kuuza nchini
Oman," alifafanua Pardhan
No comments:
Post a Comment