Habari za Punde

Zanzibar kuabndaa mpango madhubuti katika masuala ya usafiri ili kuondokana na foleni

 Na Saadam Seif

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrick Ramdhan Soraga amesema kuandaa mipango ya kitaalamu ya mipango miji ni muhimu katika kuimarisha shughuli mbali za kimaendeleo  nchini.

Ameyasema hayo wakati akizungumza  na wataalamu wa kuandaa mipango miji kutoka katika kampuni ya IDOM iliyopo Nchi Hispania huko  ofisini kwakwe Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib ‘B’ Unguja.

Katika kikao hicho kilikuwa na lengo la kujadili namna Serikali na wadau wa mipango Miji wanaweza kushirkiana katika kuandaa mipango madhubuti ya miji katika masuala ya usafiri hapa Zanzibar, Waziri Soraga amesema utekelezaji huo utasaidia kuimarisha shughuli za Uchumi kwa kuwarahisishia wananchi kufanya shughuli zao kwa ufanisi na haraka zaidi.

Aidha ameongeza kuwa Zanzibar ni Nchi inayoendelea kwa kasi kubwa hivyo suala la usafiri linahitaji kuangaliwa kwa upana zaidi ili kuondoa foleni zisizokuwa na tija ambazo kwasasa imekuwa changamoto ambayo inahitaji kutatuliwa kabla ya changamoto hiyo kuwa kubwa zaidi.

Kwa upande wake Mtaalamu wa mazingira kutoka kampuni ya IDOM Nchini Hispania Carlos De Juan Fernandez amesema mpango huo utawasaidia wakaazi  wa Zanzibar kutokana na udogo wa Kisiwa cha Unguja  watu wengi wanasafiri mara kwa mara kutokana eneo moja kwenda jengine katika ufanyaji wa shughuli zao za kila siku.


Katika kikao hizcho Waziri Soraga ameagiza kukaa  pamoja baina ya wasimamizi wa maswala ya Uwekezaji na wadau wa masula ya miundombinu ya usafirishaji kutoka katika kampuni ya IDOM iliyopo Nchini Hispania ili kujadili namna ya kutekeleza azma ya wawekezaji hao katika kuandaa mpango madhubiti wa kuimarisha mipango miji itakayorahisisha masuala ya usafirishaji nchini kwa lengo la kuchochea ukuwaji wa uchumi nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.