Habari za Punde

DKT. NCHEMBA: SERIKALI KUONGEZA BAJETI YA ELIMU

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) akitoa maelezo namna Serikali inavyotoa kipaumbele kwenye masuala ya elimu katika Bajeti zake wakati wa kilele cha mkutano wa WireED, uliojadili namna ya kuboresha elimu duniani kwa kuwekeza rasilimali fedha, uliofanyika Mjini Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu.
RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Global Partnership foe Education (GPE) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango-Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali, wakati wa kilele cha mkutano wa RewirEd uliojadili namna ya kuboresha elimu, uliofanyika Mjini Dubai, Falme za nchi za Kiarabu.

Na Benny Mwaipaja, Dubai

SERIKALI ya Tanzania imeihakikishia Jumuiya ya Kimataifa kwamba itaendelea kuwekeza rasilimali fedha kwa ajili ya kuendelea elimu ili kuwa na jamii iliyoelimika kwa ajili ya kuimarisha rasilimali watu watakaochangia maendeleo ya nchi.

Ahadi hiyo imetolewa mjini Dubai na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwenye kilele cha mkutano unaohusu uwekezaji kwenye sekta ya elimu katika karne ya 21 hasa baada ya janga la ugonjwa wa UVIKO-19 kuzitikisa nchini nyingi duniani.

Dkt. Nchemba amesema kuwa Serikali itaendelea kuongeza Bajeti ya Sekta ya Elimu kila mwaka kadri rasilimali fedha inavyopatikana na kuiomba jumuiya ya kimataifa kuchangia juhudi hizo za Serikali.

Alisema kipaumbele cha Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuhakikisha kuwa kila mtoto anayetakiwa kwenda shule anapata elimu bila vikwazo kwa kutoa elimu bila malipo huku akiboresha mazingira ya shule nchini kote.

Pause

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa nchini Tanzania kuna utashi wa kisiasa wa kuendeleza elimu ambapo bajeti ya elimu imekuwa ikiongezeka kila mwaka na mpaka sasa imefikia zaidi ya asilimia 17 na kwamba huenda siku zijazo ikafikia asilimi 20 ya bajeti yote ya Serikali.

Pause

Mkutano wa masuala ya elimu ujulikanao kama WirED umewashirikisha wadau mbalimbali kutoka duniani kote ambapo hoja mbalimbali za kuboresha elimu, ikiwemo kuwawezesha vijana, na kuimarisha masuala ya teknolojia yamejadiliwa kwa kina katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.