Habari za Punde

Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Bi. Suzan Kunambi Ametembelea Kituo cha Afya Bumbwisudi

Mkuu wa Wilaya ya Magharibi "A" Unguja Bi. Suzan Kunambi  amefanya ziara ya kikazi kutembelea Kituo cha Afya cha Bumbwisudi kujionea utendaji wa utoaji wa huduma kwa Wananchi wanaofika katika kituo hicho kupata huduma za afya.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi "A" Unguja Bi.Suzan Kunambi akimsalimia mmoja wa Watoto akiwa amebebwa na Mama yake wakisubiri kupata huduma katika Kituo cha Afya Bumbwisudi, akiwa katika ziara yake kujionea utendaji wa kazi na utoaji wa huduma ya afya kwa Wananchi wa Kijiji hicho na cha jirani.
Mkuu wa Wilaya ya Magharibi "A" Unguja Bi.Suzan Kunambi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakati wa ziara yake kutembelea Kituo cha Afya cha Bumbwisudi. 
Wananchi wa Kijiji cha Bumbwisudi Wilaya ya Magharibi "A" Unguja  wakiwa katika Kituo cha Afya cha Bumbwisudi wakisubira kupatiwa huduma ya Afya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.