Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi ashiriki maziko ya marehemu Mwanajuma Mrisho katika Masjid Mabluu Mfereji wa Wima

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Sheikh Khalid Ali Mfaume baada ya kumalizika kwa Sala ya Jeneza kumsalia marehemu Mwanajuma Mrisho, iliofanyika katika Masjid Mabluu Mfereji wa Wima na (kushoto kwa Rais) Mtoto wa marehemu Khamis Iddi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana na (kulia kwa Rais) Katibu wa Mufti Sheikh.Khalid Ali Mfaume.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutowa mkono wa pole kwa Ndugu na Familia ya Marehemu Mwanajuma Mrisho, alipofika nyumbani kwa marehemu Kijangwani Wilaya ya Mjini kutowa mkono wa pole kwa kufiwa na mzazi wao.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua baada ya kutowa mkono wa pole kwa Ndugu na Familia ya Marehemu Mwanajuma Mrisho, alipofika nyumbani kwa marehemu Kijangwani Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa wanafamilia leo 2-12-2021.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.