Habari za Punde

Viongozi na watendaji SMZ wapatiwa mafunzo ya uandaaji wa Sera

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa sera yalioandaliwa na Uongozi Institute kwa ajili ya kuwajengea uelewa Viongozi na watendaji wa serikali mafunzo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Goden Tulip Uwanja wa Ndege.

Washiriki wa mafunzo ya uwandaaji wa sera yaliowashirikisha mawaziri, Makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu wakiskiliza Mhe. Hemed wakati akiyafungua rasmi mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanjawandege.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo akimueleza Makamu wa Pili wa Rais juu ya mikakati inayochukuliwa na taasisi hiyo katika kuwajengea uwezo viongozi wa Tanzania na Barani Afrika katika kufikia maendeleo endelevu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo akimueleza Makamu wa Pili wa Rais juu ya mikakati inayochukuliwa na taasisi hiyo katika kuwajengea uwezo viongozi wa Tanzania na Barani Afrika katika kufikia maendeleo endelevu.
 

Na Kassim Abdi, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameipongeza Taasisi ya Uongozi (UONGOZI INSTITUTE) kwa kuendelea kujitolea katika kuwapatia mafunzo viongozi na watendaji wa SMZ kupitia semina mbali mbali wanazoziandaa.

Mhe. Hemed alieleza hayo wakati akiyafungua mafunzo ya uwandaaji wa sera yaliowashirikisha mawaziri, makatibu wakuu na manaibu makatibu wakuu yaliofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Jijini Zanzibar.

Alisema taasisi ya uongozi imekuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia semina elekezi wanazozitoa kwa viongozi na watebdaji wa serikali.

Makamu wa Pili wa Rais alisema nchi haiwezi kuwa na sheria ambayo haielekezi katika kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia sera zinazotengenezwa na taasisi husika.

Mhe. Hemed aliwataka washirki wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu kwa lengo la kujenga uwelewa wa pamoja utakaowasaidia kutengeneza sera bora mara baada ya mafunzo hayo.

 “Niwaombe tushiriki kikamilifu ili kujenga uelewa wa pamoja” Alisema Makamu wa Pili wa Rais

Nae, Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said alisema mafunzo hayo yamaeandaliwa kwa lengo kujenga uwelewa kwa watendaji juu ya  uwandaji wa sera mbali mbali katika taasisi za serikali.

Alieleza kuwa, kupitia mafunzo hayo washiriki wataanza na utengenezaji wa sera ya uchumi wa Buluu kwa vitendo sekta ambayo serikali imeweka kipau mbele katika kukuza uchumi wake.

Kwa upende wake Katibu Mkuu wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la wawakilishi Thabit Idarous Faina alisema kwa sasa serikali imeandaa utaratibu maalum wa ufuatiliaji wa uwandaaji wa sera ili kupata sheria nzuri zitakazokuwa na mpango kazi kwa ajili ya kurahisha utekelezaji wake.

Taaisi ya Uongozi imeanzishwa mwaka 2010 ikiwa na lengo kuwasaidia viongozi wa Tanzania na Barani Afrika kwa Ujumla kufikia maendeleo endelevu sambamba na kufanya tafiti kwa ajili kuwezesha utekelezaji wa sera mbali mbali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.