Habari za Punde

Waziri Simai atoa pole kwa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said amefika katika Ofisi za Makao Makuu ya Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Kilimani Mjini Unguja, na kuonana na Kamishna wa Kikosi hicho Rashid Mzee Abdallah, kwa lengo la kutoa pole kwa Mkuu wa Kikosi hicho kufuatia kutokea kwa ajali ya moto katika Ghala la la kuhifadhia vifaa mbalimbali na kupelekea kifo cha Askari mmoja wa kikosi hicho. 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said akizungumza na kutowa mkono wa pole kwa Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Zanzibar (kulshoto kwake) baada ya kutokea kwa ajali ya moto na kupoteza askari wake katika ajahi hiyo, na (kulia kwake) Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Masoud Ali Mohammed, wakitembelea katika ghala iliyopota ajali hiyo ya moto. 

Mhe Simai akiwapa pole Askari wote wa kikosi hicho kwa kupoteza mwenzao pamoja na familia na kuwaomba kuwa na subira katika msiba huo.

Katika ziara hiyo Mhe Simai amekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe Masoud Ali Mohammed.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.