Habari za Punde

RC Ayoub afanya ziara ya kushtukiza sehemu zinazopiga mziki Nungwi na Kiwengwa

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub M. Mahmoud amefanya operesheni za kustukiza usiku wa kuamkia leo katika maeneo mbali mbali yanayopiga mziki katika maeneo ya Nungwi na Kiwengwa.

Operesheni hiyo  imelenga kulinda na kurudisha hali ya usalama kwa utalii na utulivu na kudhibiti vilivyo vitendo vya udhalilishaji na matumizi ya madawa ya kulevya.

Operesheni ilianza kuanzia saa sita na robo usiku na kumalizika majira saa kumi na nusu ni hatua ya awali ya kusimamia na kukagua mienendo maeneo yanayopiga miziki katika mkoa huo, ambapo tayari Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Unguja imeshatoa barua za onyo na kuwakumbusha wamiliki wa maeneo hayo kufanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria.

Mhe. Ayoub M. Mahmoud amesema operesheni hio itaendelea kwa namna nyengine mara kwa mara na kuwataka kutojaribu kudharau onyo la serikali kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.