Habari za Punde

Wanafunzi skuli ya Sekondari Shamiani washiriki na kushinda katika mashindano ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa na Wanafunzi Nuwairat Yussuf Salim na Khelef Mohd Nassor ambao ni Wanafunzi wa kidato cha sita kutoka Skuli ya Sekondari Shamiani ambao wameshiriki katika mashindano ya Wanasayansi Chipukizi Tanzania "Young Scientists Tanzania" na kufanikiwa kushinda katika kipengele cha National Institutes of medical research na kuchaguliwa kuwa mradi bora katika kipengele hicho.

Mwalimu wa Skuli wa Wanafunzi hao mwalimu Masoud Salim Ali amesema mradi wao unaosema (impacts of seaweed farming on coastal forest of Pemba) ikiwa na maana athari ya zao la mwani katika misitu ya mwambao wa bahari ya Pemba.
Amesema awali mashindano hayo yalihusisha Skuli 10 kwa Pemba na 20 Unguja na kufanya maonyesho ya mashindano ambapo Skuli ya Shamiani ilifanikiwa kuingia katika mashindano ya Kitaifa ya Tanzania ambayo yalitakiwa yafanyike October lkn kutokana na tatizo la covid-19 mashindano hayo yalifanyika kwa njia ya mtandao kwa kushindanisha Mikoa 25, Skuli 238 na Projects zisizopungua 578.
Amefahamisha kuwa mradi huo umeshinda kutokana na upekee na utafauti wa miradi yote ambayo wameshindana nayo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.