Habari za Punde

ZIARA YA MHE MARY MASANJA EXPO 2020 DUBAI LEO DESEMBA 16,2021

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi wa banda la Ethiopia, Bi. Haimanot Kassave (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu bidhaa zinazopatikana katika banda lao kwenye Maonesho ya Dunia ya Expo 2020 Dubai. Kushoto ni   Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi, Balozi Edwin Rutageruka

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) leo Desemba 16,2021 ametembelea mabanda ya nchi za Uganda, Burundi, Ethiopia na Kisiwa cha Malta kwa lengo la kujifunza namna ambavyo nchi hizo zimeshiriki katika maonesho ya Expo 2020 Dubai.

Katika ziara hiyo, Mhe. Mary Masanja aliongozana na Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi, Balozi Edwin Rutageruka, Mkurugenzi wa Banda la Tanzania kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Getrude Ng’weshemi kutoka TanTrade  na Afisa Masoko Mkuu kutoka  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Michael Makombe

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akipokea kikombe cha kahawa kutoka kwa mshirikiwa maonesho alipotembelea banda la Ethiopia kwenye Maonesho ya Dunia ya Expo 2020 Dubai. Kulia ni Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi, Balozi Edwin Rutageruka .

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.